Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Imefichuka! Ugomvi wa Gigy na MO J ni kiki

MO NA GIGY Imefichuka! Ugomvi wa Gigy na MO J ni kiki

Mon, 27 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Siku chache baada ya kuibuka kwa bifu zito kati ya Gigy Money na mzazi mwenzake MO J, imebainika kuwa huwenda ishu hiyo ikawa ni kiki.

Hii ni kutokana na wawili hao kila mmoja kumposti mwenzake na kumuandikia mambo mazuri ghafla tofauti na ilivyokuwa inatarajiwa kwa watu ambao walitukanana matusi mazito halafu ghafla kubadilika.

"Ni kiki tu ile na sio ishu seriuos, angali Gigy kaachia ngoma na MO J amemsapoti," kimeeleza chanzo makini.

Gigy ameandika waraka mreefu kwenye Insta story yake akidai kuwa amemsamehe mzazi mwenziye huyo na kwamba hakuna mshindi katika sakata lao na kwamba yameisha.

Wiki iliyopita kilisambaa kipande cha video kilichomuonesha MO J akiwa amekwenda nyumbani kwa Gigy na kukiwasha ile mbaya huku Gigy akidai anakwenda polisi kumshtaki kwa kufanyiwa vurugu nyumbani kwake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live