Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Idriss Sultan kortini tena

A5df3ada94ebd6c05c5c7b5eefd7a676 Idriss Sultan kortini tena

Tue, 28 Jul 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MSANII wa vichekesho, Idriss Sultan (27) na wenzake wawili wamesomewa upya mashitaka ya kuchapisha maudhui bila leseni ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kumuachia na kukamatwa tena.

Mbali na Idriss ambaye ni Mkazi wa Mbezi Beach jijini Dar es Salaam, washitakiwa wengine ni Mkazi wa Msasani Dokta Ulimwengu (28) na Msanii na Mkazi wa Gongo la Mboto, Isihaka Mwinyimvua(22).

Washitakiwa hao awali walifikishwa mahakamani hapo na kusomewa mashitaka hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi. Jana, kesi hiyo iliitwa kwa ajili ya washitakiwa kusomewa maelezo ya awali lakini upande wa mashitaka ulidai bado hawajakamilisha kuandaa maelezo hayo.

Hata hivyo, Hakimu Shaidi alifuta kesi hiyo na washitakiwa walikamatwa na kusomewa upya mashitaka yao. Wakili wa Serikali, Adolf Ulaya alidai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Yusto Ruboroga kuwa washitakiwa wanadaiwa kutenda kosa hilo kati ya Machi 8, 2016 na Machi 12, 2020 maeneo ya jiji la Dar es Salaam.

Alidai washitakiwa hao walichapisha maudhui kupitia chaneli ya Local Motion ya YouTube bila kuwa na leseni ya TCRA.

Habari zaidi soma HabariLEO kesho.

Chanzo: habarileo.co.tz