Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Idris Sultan, mwenzake wajadiliana na DPP kumaliza kesi

Idris+pic Idris Sultan, mwenzake wajadiliana na DPP kumaliza kesi

Wed, 5 Aug 2020 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

By Pamela ChilongolaDar es Salaam. Upande wa utetezi katika kesi inayomkabili mchekeshaji Idris Sultan na mwenzake Innocent Maiga umedai kuwa washtakiwa hao wapo kwenye mazungumzo na Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Tanzania (DPP), kwa ajili ya kuomba msamaha na kukiri makosa yanayowakabili.

Washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka mawili likiwemo la kushindwa kufanya usajili wa laini ya simu ambayo ilikuwa inamilikiwa na mtu mwingine kinyume cha sheria.

Hatuna hiyo imekuja baada ya wakili wa Serikali, Kijja Luzingana kudai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu, Rashid Chaungu kuwa shauri hilo lilikuja katika mahakama hiyo kwa ajili ya kusikikilizwa ushahidi.

"Leo tuna shahidi mmoja na tupo tayari kuendelea na ushahidi,"alidai Luzingana ndipo wakili wa utetezi, Francis Mwakifuna alidai washtakiwa hao wapo kwenye mazungumzo  kwa ajili ya kuomba msamaha na kukiri makosa yanayowakabili.

"Wakili anayeendesha shauri hilo yupo katika Mahakama ya Rufaa na tumeleta hoja za kuomba msamaha na kukiri makosa yanayowakabili, hivyo tupo kwenye mchakato," alidai Mwakifuna.

Hakimu Chaungu aliutaka upande wa utetezi kabla ya Agosti 27, 2020 uwe umeshawasiliana na wakili wa Serikali na utakapofika mahakamani tarehe hiyo uwe na majibu.

Chanzo: mwanaspoti.co.tz