Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Idris Sultan ametangaza kuingiza filamu nyingine Netflix

Idrss Pic Idris Sultan ametangaza kuingiza filamu nyingine Netflix

Mon, 30 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Muigizaji maarufu wa Bongo Movies, Idris Sultan ametangaza kuingiza filamu nyingine katika platform ya Netflix.

Hii inakuwa ni filamu ya pili kwa mkali huyo kuingia katika jukwaa hilo kubwa na maarufu ulimwenguni naye akishiriki.

Filamu yake ya kwanza ilikuwa ni "Slay" ambayo iliingia kwenye jukwaa hilo mwaka 2021.

Filamu hii ya pili inaitwa "Married To Work" ambayo inatarajiwa kuonekana ndani ya jukwaa hilo February 10, 2023 ambapo waigizaji wengine ni kutoka Kenya na Nigeria.

Aidha, filamu ya Kitanzania ambayo pia ilishawahi kuingia katika jukwaa hilo ni "Binti" ambayo imeongozwa na Mtanzania Seko Shamte.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live