Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Idris Sultan afunguka sababu za kushuka kwa ubunifu

Idriss Sultan Idris Sultan.

Wed, 5 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Muigizaji na Muongoza Filamu Mashuhuri nchini Tanzania, Idris Sultan amekiri kuwa ubunifu katika uzalishaji wa Filamu na Tamthilia bora nchini Tanzania, unabanwa na wenye visimbuzi ambao ndio wanunuaji wakubwa wa kazi za Filamu na Tamthilia nchini Tanzania.

"Nchini Tanzania, waongozaji wote wa Filamu na Tamthilia wanauza Filamu zao kwa visimbuzi vitatu tu, hivyo kuna namna wanabanwa katika ufanyaji wa kazi zenye ubunifu mkubwa sababu, hata wanaonunua kazi zao, pia wanaangalia watazamaji wanapenda Filamu za aina gani hivyo hata filamu zinazonunuliwa zinakuwa za aina moja.

Ukitazama kwenye visimbuzi vyote utagundua kuna utitiri wa Filamu na Tamthilia zenye maudhui ya kufanana Kwa kiwango kikubwa kwani nyingi zinalenga mambo ya Mahusiano ya kimapenzi, migogoro ya familia na jamii.

Waongozaji wa filamu na Tamthilia wa Tanzania wanashindwa kuandaa filamu za maudhui ya ubunifu mkubwa na yenye utofauti sababu ya aliyeshika shilingi ndiye anayesema nini kifanyike na nini kisifanyike Kwa wakati upi," amesema Idris Sultan.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live