Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Idadi ya wanawake wanaovuta sigara yaongezeka

Idadi Ya Wanawake Wanaovuta Sigara Yaongezeka Idadi ya wanawake wanaovuta sigara yaongezeka

Tue, 21 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Uvutaji wa sigara ni hatari kwa afya yako” ni tangazo marufu lililopo maeneo mengi.

Licha ya uwepo wa matangazo hayo na kutolewa kwa elimu katika vyombo vya habari, kuhusu athari za matumizi ya sigara, baadhi ya wanawake wameendelea kujiingiza katika uvutaji wa sigara huku wanaume wakipungua; utafiti unaeleza.

Ripoti ya utafiti wa Afya ya Uzazi na Mtoto na Viashiria vya Malaria (THDS) ya mwaka 2022 iliyotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), inaeleza kuwa kiwango cha wanawake wanaovuta sigara ni asilimia moja.

Kiwango kimeendelea kubaki hivyo licha ya idadi ya watu katika vipindi tofauti vya kuongezeka, jambo linaloashiria kuongezeka wa idadi ya wanawake wanaovuta sigara kati ya 2017 na 2022.

Kabla ya takwimu hizo za NBS, mwaka 2021 shirika la Afya Duniani (WHO) likishirikiana na Serikali ya Tanzania walitoa takwimu ya ongezeko la wanawake kuvuta sigara, kwa kueleza kuwa mwaka 2012 walikuwa asilimia 2.9 na mwaka 2018 walikuwa asilimia 3.2.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live