Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ibrahh: Sijalipwa pesa zangu miezi 8 sasa

Ibraah M (11).jpeg Msanii Ibrahh.

Tue, 26 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanamuziki kutoka Lebo ya muziki ya Konde Gang, Ibraah amesema kuwa kwa sasa anapitia hali ngumu kwenye muziki wake.

Ibrah ambaye ni first born wa lebo hiyo inayomilikiwa na Harmonize, amesema kuwa hajalipwa pesa zake kwa muda mrefu jambo linalosababisha maisha yake yawe magumu kupindukia.

"Ni kweli hali yangu siyo nzuri kimaisha na kimuziki kwasababu nafanya kazi lakini silipwi pesa zangu, ni miezi nane sasa hivi Ziiki hawajanilipa na uongozi wangu uko kibiashara zaidi ndiyo maana nimekaa miezi sita bila kutoa wimbo kwa sababu nyimbo nilizotoa hazirejeshi mapato hii inafanya maisha yangu yazidi kuwa magumu.

"Licha ya kutokulipwa lakini watu wamekuwa hawanioni kwenye show kwasababu mapromota wanashindwa kufikia dau langu, mimi ni Expensive sana lazima nilipwe pesa nyingi ndiyo maana hata kwenye ubalozi wa makampuni hamnioni, watu wengi wananishindwa kutokana na gharama zangu kuwa Expensive," amesema Ibraah.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live