Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ibraah msanii bora chipukizi 2020

9ec6a1f6f48e5c86accef689c6362e99 Ibraah msanii bora chipukizi 2020

Mon, 21 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MSANII wa muziki wa Bongo fleva amepewa tuzo ya msanii chipukizi wa mwaka 2020 na kipindi cha Empire cha E FM Radio.

Ibraah ambaye yupo chini ya lebo ya Konde Music Worldwide akiwa msanii wa kwanza kusainiwa na lebo hiyo inamilikiwa na Rajabu Abdul ‘Harmonize’ mwaka huu aliachia EP yake inayoitwa Steps.

Akizungumza katika kipindi cha Empire, Ibraah alikishukuru kituo hicho kwa kutambua mchango wake.

“Nashukuru kwa kutambua mchango wangu katika tasnia, najua bado nina safari ndefu lakini tuzo kama hizi zitakuwa zinanifanya niongeze bidii.

Kabla ya kuingia kwenye muziki Ibraah alisema alikuwa anauza CD lakini baada ya kupata mtaji wa kutosha alianza kuuza makoti.

Hadi sasa Konde Music ina wasanii watano ambao ni Ibraah, Country Boy, Cheed, Killy na Skales kutokea nchini Nigeria.

Chanzo: habarileo.co.tz