Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

INSTAGRAM: Alikiba amewaomba msamaha mashabiki wake

673 CaptureWEE TZW

Wed, 27 Dec 2017 Chanzo: millardayo.com

December 1 2017 Mkali kutoka Bongoflevani Alikiba Kupitia Jiwe la mwezi Singida aliwatangazia mashabiki zake kuwa Dec 26 2017 atazindua Product yake na Pia wajiandae kwa ajili ya funga mwaka na King Kiba, December 27 2018 ameutumia mtandao wake wa Instagram kuwaomba msamaha mashabiki zake kwa kutoweza kutimiza ahadi hizo.

Post ya kwanza ya Alikiba ilisomeka>>>officialalikibaHello fans, natumaini kila mmoja wenu amekuwa na wakati mzuri katika kipindi hiki cha sikukuu. Ningependa kuchukua nafasi hii kuwaomba radhi kwa kushindwa kuwatimizia ahadi ya kufanya #FungaMwakaNaKingKiba kama ambavyo niliwatangazia mwanzo. Haikuwa lengo langu ila kuna mambo yamejitokeza yaliyo nje ya uwezo wangu ambayo yamesababisha kutoweza kufanyika kwa tukio letu ambalo pia lingehusisha uzinduzi wa products zangu pamoja na wimbo wangu mpya. Hata hivyo hivi karibuni Mungu akijaalia nitawapa taarifa ya namna tutakavyoufungua Mwaka! Asanteni kwa ushirikiano na support mnayonipa kila siku. : In the other news…..Kigali, come party with King on the 1st of January 2018 at Amahoro Stadium. #FunguaMwakaNaKingKiba

Post ya pili ilisomeka>>>nilitakiwa kujiunga na mashabiki wangu wa chato GEITA Nyumbani Kwa Baba yetu muheshimiwa Rais lakini nilishikwa na homa Kali ila leo naendelea Vizuri samahani kwa kutokuwepo lakini nawaahidi nitarudi tena kwa nguvu zote MUNGU akipenda hivi karibuni tutawaandalia show ya kipekee lakini vilevile @officialabdukibaa Mdogo Wangu aliniwakilisha vema namshukuru sana nawatakia sikukuu njema

#SupportedByKiba

#KingKiba

 

 

Chanzo: millardayo.com