Mkurugenzi wa kituo cha EFM na TV Majizzo ametangaza rasmi kumjumuisha kwenye timu ya ya Watangazaji wa Joto la Asubuhi Mtangazaji mpya Roland Barnabas alimaarufu kama Madenge.
Madenge ambaye amejipatia umaarufu mkubwa kupitia Twitter amejiunga rasmi na EFM akiwa kama mmoja ya Watangazaji wa kipindi cha Joto la Asubuhi.
Madenge wengi wanamfahamu kama Banker yaani mtu aliyekuwa anafanya kazi bank. Kupitia ukurasa wake wa Twitter ameandika haya:
“Nimekaa benki miaka 5, nilianzia branch na kupitia ukurasa huu huu wa twita nikahamishiwa HQ kitengo cha Marketing and communications. Leo nimejiunga @EfmTanzania creative marketing and radio presenter. Asante @officialmajizzo kwa kuniamini.”
Baada ya kuodoka Maulid Kitenge na Gerald Hando warithi wao ni Masanja Mkandamizaji kwa kusoma magazeti na bwana Madenge.