Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Huyu ndo Jeniffer Kanumba tuliyemtaka

Jeniffer Kanumba Sgrs Huyu ndo Jeniffer Kanumba tuliyemtaka

Fri, 6 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Anaitwa Hanipha Daudi maarufu kama Jeniffer Kanumba, ni Mwigizaji wa Bongo Movie nchini.

Alianza kuonekana kwenye Filamu za Marehemu Steven Kanumba na moja ya Filamu iliyompatia umaarufu mkubwa ni Filamu ya (Uncle JJ) Filamu ambayo ilichezwa kwa umakini mkubwa.

Kama ingekuwa kwenye zama hizi za kidigitali basi ingevuna mamilioni ya pesa na miongoni mwa wahusika walioinogesha Filamu hiyo ni Jeniffer Kanumba.

Baada ya Filamu zake za utotoni kuwavutia watu wengi na jina lake kuwa miongoni mwa majina makubwa Afrika Mashariki, wengi walitarajia ataenda na uwezo ule hata atakapokuwa mkubwa, atakuwa Mwigizaji namba moja Tanzania pengine hata Afrika.

Lakini matarajio yamekuwa ndivyo sivyo Jeniffer anayeonekana sasa siyo yule aliyedhaniwa angekuwa.

Nadhani tunamuona Elizabeth Michael Lulu jinsi alivyoushikilia umaarufu wake, licha ya kupitia misukosuko mingi akiwa na umri mdogo ikiwemo kukaa gerezani lakini amekuwa strong kwenye kazi yake, ameweza kuishikilia kazi na kuushikilia umaarufu kwa wakati mmoja na amefanikiwa.

Leo hii Lulu anapata madili makubwa kutoka kwenye makampuni mbalimbali, analipwa pesa nzuri kwenye Filamu anazocheza, Lulu akipita mtaani macho yote kwake.

Jeniffer Kanumba amekwama sehemu, ameshindwa kuubeba umaarufu na kazi kwa wakati mmoja, anaonekana kwenye Tamthilia kadhaa lakini si kwa ukubwa ule anaotakiwa kuwa nao, watu hawamfatilii tena kwa ukubwa kama zamani.

Huenda ndiyo aina ya maisha aliyoichagua yeye ya kutotaka kufatiliwa lakini kwa kipindi hiki ambacho umaarufu ni pesa anawezaje kushindwa kuchangamkia nafasi hii.

Popote alipo ajue kwamba anawanyima mashabiki zake uhondo wa kipaji alichonacho, nafasi bado ipo tena kubwa.

Yote kwa yote bado tunampenda, tunamuombea na tunamtakia kheri za mafanikio zaidi, apate kazi zaidi za kitaifa na kimataifa lakini pia aendelee kukaa karibu na Mungu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live