Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Huyu ndiye Abaeme Onyinye Stellamaris

Abaeme Onyinye Stellamaris Abaeme Onyinye Stellamaris

Sat, 29 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wapo baadhi ya watu ambao hupata na uwoga baada ya kutazama movie fulani ya kutisha au zinazoonesha vidonda kupita kiasi, licha ya kuwa wanafahamu ni movie na siyo uhalisia.

Ili mtunzi aweze kusema kazi yake imefanikiwa ni lazima iweze kuteka hisia za watu, moja ya kitu ambacho huchochea kuteka hisia hizo za watazamaji ni muonekano wa mhusika.

Abaeme Onyinye Stellamaris, kutoka nchini Nigeria ni Arseface Make-up artist ( film make-up artist) ambaye kazi yake kubwa huwa ni kuhakikisha muonekano wa mhusika kwenye filamu unaonekana kama uhalisia.

Arseface make-up ni kitu gani? 

Ni make-up za kutisha zenye kubadilisha sura ya mtu na kuwa na muonekano mwingine, kama vile zombie na majeraha.

Akizungumza na Mwananchi, Obaeme ambaye ndiye mpakaji wa make-up amesema alianza kazi hiyo mwaka 2018, akiwa hajui chochote kuhusu aina hizo za make-up. 

“Mwanzo nilikuwa sijui kitu nikawa nikiangalia Movie za Kimarekani najiuliza inakuwaje mtu anabadilishwa sura na kuwa ya kutisha na inakuwaje anaonekana na vidonda,” amesema.

Amesema kutokana na maswali hayo ambayo amekuwa akijiuliza ndipo akaanza kutaka kujua namna ambavyo watu wanabadilishwa hadi kuwa na muonekano mwingine.

“Kipindi hicho nilikuwa najua kupaka aina nyingine za make-up kama vile beauty make-up, editorial make-up, ilinibidi nianze kujifunza jinsi ya kutengeneza make-up za kutisha kupitia mtandao wa YouTube kwa sababu nilikuwa sina pesa ya kujifunza ilikuwa ni gharama sana,” amesema

Aidha amesema kuwa baadaye alifanikiwa kupata elimu kuhusu kupaka make-up hizo,Canada jambo lililoweza kusaidia apate uelewa mpana zaidi.

Amesema vifaa vinavyotumia kutengenezea make-up hizo huuzwa kwa gharama kuwa huku akivitaja kama vile silicone ya make-up, powder.

Mbali na hayo ameeleza kuwa changamoto kubwa ambayo anakutana nayo kwenye kazi ni baadhi ya waigizaji kuwa na masharti mengi wanapofanyiwa make-up.

“Nakutana na changamoto kutoka kwa waigizaji baadhi wana tabia ya kunipangia wao wanataka nini, yaani ni wabishi,” amesema.

Anasema kazi anayofanya imekuwa ikiwashangaza watu wengi kwani hata kwa Nigeria bado haijafahamika sana, licha ya kuwa amefanya make-up za aina nyingi amesema ubunifu wa mazombi ndiyo humvutia zaidi.

“Katika kazi zangu zote napenda kutengeneza mazombi yaani kwa kifupi napenda kutengeneza mtu aonekane awe wa kutisha,” amesema.

Kati ya movie ambazo mkono wake umehusika kuwafanyia waigizaji ubunifu ni  ‘Far from home’, ‘Setup 2’, ‘Eagle Wings’, ‘Sugar na nyinginezo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live