Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Huyu ndio mtu mwenye ushawishi zaid Duniani

Shah RUKH Khan.jpeg Shah Rukh Khan

Tue, 11 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shah Rukh Khan ameshika nafasi ya 1 katika jarida kongwe na maarufu la "Time" la nchini Marekani kama mtu mwenye ushawishi zaidi duniani kwa mwaka 2023 ambapo wasomaji zaidi ya milioni 1.2 wa jarida hilo ndio wamepiga kura kupata orodha ya watu 100 wenye ushawishi zaidi duniani.

Nafasi ya 2 wamepigiwa kura wanawake wa nchini Irani ambao kwa miezi sasa tangu september mwaka jana wamekuwa katika maandamano miji tofauti nchini Irani na ughaibuni kudai uhuru wa haki zao na maisha yao katika taifa hilo linaloongozwa kwa sheria za kiislamu.

Ni baada ya kifo cha utata cha mwanadada Mahsa Amin(22) aliyefariki 16 September 2022 mikononi mwa polisi wanaoitwa wa kulinda maadili baada ya kumkamata Mahsa Amin kwa madai alikuwa hajavaa hijabu inavyotakiwa kwa mujibu wa sheria za kiislamu, Mahsa alifariki baada ya kudaiwa kupigwa kichwani na Polisi baada ya kumuweka kizuizini kwa siku kadhaa, hali hiyo iliibua hasira kubwa kwa wanawake wa taifa hilo la kiislamu wakitaka wawe huru na maisha yao hadi sasa hawajapoa huku wakiungwa mkono na Diaspora.

Nafasi ya 3 wamepigiwa kura Wafanyakazi wa sekta ya afya Duniani kote, Nafasi ya 4 wamepigiwa kura Meghan Markle na Prince Harry ambao miezi ya karibuni biography ya Harry na docuseries yao viliibua mambo kadhaa ikiwemo kuilipua familia ya kifalme Uingereza anakotokea Prince Harry.

Katika nafasi ya 5 wasomaji wamempigia kura Lionel Messi(35) aliyeisaidia nchi yake kutwaa kombe la Dunia 2022 Orodha kamili ya watu 100 wenye ushawishi itatolewa April hii na jarida la Time, miongoni mwa waliopigiwa kura katika orodha hiyo ni pamoja na Beyonce, Rais wa Brazil, Serena Williams na wengineo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live