Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Huyu nd'o staa aliyemkutanisha Dimpoz na Ronaldo

OMMY DIMPOZ BAILY Huyu nd'o staa aliyemkutanisha Dimpoz na Ronaldo

Mon, 29 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Staa wa Bongo Fleva Ommy Dimpoz ambaye amekuwa gumzo kwa watu wengi kuonekana akipata nafasi ya kupiga picha na wachezaji wakubwa wa soka wa Man United kama Cristiano Ronaldo, Jadon Sancho, Bruno Fernandez na David De Gea leo ameweka wazi connection hiyo kaipata wapi.

Ommy Dimpoz ameeleza kuwa aliyempa fursa hiyo ya kufika katika parking ya wachezaji wa Man United na kupiga nao picha ni staa wa Timu ya Taifa ya Ivory Coast anayecheza Man United Eric Bailly ambaye nae alikutanishwa nae na Mwana FA.

Ommy ameeleza hayo na kupost kuwa kila kitu kwenye maisha ni connection, kwa sasa Bailly anaondoka Man United na kwenda kwa mkopo wa muda mrefu katika club ya Olympic Marseille ya Ufaransa.

“Goodluck to My Brother @ericbailly24 on his New Chapter @olympiquedemarseille

Mh Mbunge @mwanafa Alinitambulisha kwa Eric, Eric akanitambulisha kwa Wachezaji wote wa Man U yani wameniunganisha mpaka kwenye Group lao la Whatsaap VIJANA Maisha ni Connection Japo Siwakubali Uto ila ukitaka kupiga picha na @caamil_88 @hajismanara @mayelefiston Njoo Ofisini kwangu GSM na Mimi ntakupeni Connection”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live