Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hussein Machozi awaka wanaosema kuwa 'ameolewa'

Hussein Machozi Mzunguz Hussein Machozi.

Fri, 3 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva nchini Tanzania ambaye kwa sasa anaishi nchini Italia, Hussein Machozi amewataka Wabongo kutomchukulia poa kisa tu ameoa mwanamke mzungu wakahisi kuwa 'ameolewa' (analelewa na mwanamke huyo).

Machozi amesema kuwa Watanzania wengi wakiona unaishi na mwanamke wa kizungu kama mke na mume wanahisi kuwa huna pesa na unamtegemea mwanamke huyo.

"Watanzania wakiona mtu amepata mwanamke mwenye pesa utaambiwa umeolewa, Ben Pol aliambiwa kaolewa na mwanamke Mkenya na Dogo Janja nae aliambiwa ameolewa na Irene Uwoya, hawajui mtu ametoka nae wapi wanasema ameolewa, mimi nilienda Ulaya kwa mambo yangu"

"Hakuna mwanaume anayeolewa, wanaume wote wanaoa, Mtanzania huwa hataki kuona mtu anafanikiwa, maneno yao huwa wanayatoa Instagram wanaamini mtu akienda Ulaya anaenda kuishi vizuri," amesema Hussein Machozi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live