Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Hufurahii tendo la ndoa? Soma hapa

Hufurahii Tendo La Ndoa Hufurahii tendo la ndoa? Soma hapa

Tue, 20 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hufurahii tendo la ndoa ni miongoni mwa vitu ambavyo vinakamilisha raha ya mapenzi. Tendo hili ni muhimu, linatawisha uhusiano hata kama unakuwa unalegalega, linapofanyika kwa ukamilifu wake, uhusiano unarejea.

Apo wanaolitumia tendo hili kama suluhu pindi wanapokuwa wamegombana. Mtu anaamini anapokuwa amegomana na mwenzake, anachokifanya kikubwa ni kuhakikisha anafanya kila mbinu ili aweze kukutana kimwili na mwenzi wake na kuanzia hapo ugomvi unakuwa umekwisha.

Wataongea vizuri, watasameheana na kusahau kabisa kama walikuwa na ugomvi saa au siku chache zilizopita. Hivyo basi utakubaliana na mimi kwamba tendo hili lina faida kubwa sana katika uhusiano.

Kwa mujibu wa wataalamu mbalimbali, tendo hili pia huifanya akili kuwa ‘active’. Huifanya akili ifute mafaili ya ugumu wa maisha, mafaili ya matatizo ya kazini, hufuta kumbukumbu zote mbaya za siku.

Unapolifanya tendo lile katika kiwango cha kuridhisha, linakufanya uwe mpya. Linakupa nguvu ya kwenda kwenye mapambano mapya ya maisha na wakati mwingine kutokuwa na tamaa zisizokuwa na kichwa wala miguu.

Bahati mbaya sana, kizazi cha sasa kinakubwa na changamoto kubwa sana ya wapendanao wengi kutolifurahia tendo hili.

Wengi wetu tulanifanya ilimradi tu. Matokeo yake, tunazalisha matatizo makubwa katika maisha ya uhusiano. Wengi wanakuwa hawafurahii tendo hili.

Inapotokea mtu hafurahii tendo hili, anaweza kuvumilia kwa muda mrefu lakini siku akikutana na vishawishi vikubwa, ni rahisi sana kuangukia kwenye usaliti.

Kutofurahia tendo la ndoa kunaweza kusababishwa na magonjwa mbalimbali lakini pia kunaweza kusababisha na mambo mbalimbali ya kawaida kabisa.

Unaweza usifurahie tendo kwa sababu tu ya kuwa na tatizo la kuandaliwa au kumuandaa mwenzako vizuri.

Yawezekana pia ukawa na tatizo la kisaikolojia. Ukawa na mawazo juu ya jambo fulani, hiyo pia ni sababu kubwa ya kutofurahia tendo la ndoa. Ukiachana na yale yanayosababishwa na magonjwa, kila mmoja wetu anapaswa kuyashughulikia kwanza haya ya kawaida ambayo hayahitaji hata kumuona daktari ili aweze kukuchunguza.

Kama una tatizo la kutojiamini, lishughulikie kwa kuwa na ujasiri wakati wa tendo. Kama unahisi kuna kitu unashindwa kufanikisha, tumia mbinu mbalimbali za kumfanya mwenzi wako alifurahie tendo wakati na wewe ukiwa unafurahia.

Somo la kujiandaa linawahusu wote wawili. Mwanaume amuandae mwanamke, mwanamke pia amuandae mwanaume. Asiwepo mmoja wenu ambaye atashiriki tendo pasi na kufikia tamati ya tendo.

Kila mmoja amsome mwenzake. Ajue ni kitu gani ambacho kinampeleka karibu sana na hisia za tendo. Kifanye hicho ili kumuweka karibu na hatimaye wte mfurahie.

Hakikisha akili yako inakuwa pale wakati mnapokuwa faragha. Achana kabisa na mawazo mengine, akili yako yote iwaze tendo. Hakikisha unamweka mwenzako kwenye mudi ya kufurahia tendo kwa kufanya kila utundu.

Mshike sehemu anayopenda kushikwa. Jaribu jaribu kufanya mambo mpya kila siku ambayo yatakurahishia kujua udhaifu wa mwenzi wako uko wapi.

Ukiona hayo yote mnayafanya na bado hamfurahii tendo, unaweza kumuona daktari kwa msaada zaidi!

Chanzo: www.tanzaniaweb.live