Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Huddah akubali kuwa na mke mwenza

HUDDAH MUNROE M.png Huddah Munroe

Wed, 3 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mfanyabiashara na sosholaiti maarufu nchini Kenya, Huddah Monroe amekiri kuwa yuko tayari kuwa katika ndoa ya wake wengi.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Huddah (30) amesema kuwa atamruhusu mumewe mtarajiwa kuoa mke wa pili huku akiongeza kuwa ni sharti mwanaume awe na pesa za kutosha kabla ya kuoa mke mwingine.

"Sijali mume wangu kuoa mke wa pili ikiwa ni tajiri na anaweza kututunza, kwa sababu sifikirii kumhudumia mume wangu kwa maisha yangu yote," alisema Huddah.

Kwa kawaida, mremb huyo huwa haogopi kusema anachofikiria au kutangaza matamanio yake. Monroe huwa hajali maoni ya watu kuhusu kile anachoposti kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii.

Huku hayo yakisemwa, Huddah huwaeleza wafuasi wake kuhusu kile anachofikiria kuhusu maisha yake. Siku za hivi karibuni amekuwa akizungumzia masuala ya ndoa.

"Wakati fulani nitakuwa nimechoka, na atakuwa mzee pia, kila mmoja anachoka kadri muda unaposonga," Huddah alisema.

Kwa sasa hakuna uwazi kuhusu mahusiano ya mrembo huyo huku ikidaiwa kuwa yupo kwenye mahusiano na mkali wa muziki wa RnB kutoka Bongo, Juma Musa Mkambala almaarufu Juma Jux .

Lakini Jux aliweka wazi kuwa yeye na Huddah ni marafiki tu na hakuna uhusiano yoyote kati yao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live