Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Huddah: Mwanaume mzuri ni yule ambaye mama yake amefariki

HUdda Safi Huddah: Mwanaume mzuri ni yule ambaye mama yake amefariki

Wed, 26 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanasosholaiti Huddah Monroe amewacharukia wanaume ambao muda wote wanapenda kukaa karibu na mama zao na kusema kwamba wanaume kama hao ni vigumu sana kudumu katika mahusiano nao kwa mwanadada yeyote.

Kupitia mfululizo wa chapisho kwenye Instagram yake, Monroe alipakia video fulani ambayo ilisambazwa mitandaoni na staa wa Afropop kutoka Nigeria, Burna Boy akikumbatiana na mamake na kusema kwamba wanaume kama hao ni kibarua kigumu sana katika mahusiano.

“Huyu ni mwanaume mgumu sana kuchumbiana naye, wakati mama yake amemgandia hivi muda wote, basi sahau kabisa. Ndoa yenu haiwezi dumu,” Huddah Monroe aliandika kwenye video ya Burna Boy na Mama yake wakikumbatiana kwa furaha.

Pia alizidi kusema kwamba aliwahi ambiwa na rafiki yake kuwa mwanaume bora wa kuchumbiana naye ni yule mama yake amefariki ama yule ambaye muda wote yupo mbali sana na mama mzazi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live