Dar es Salaam. Kitendo cha msanii Harmonize kuandika barua kutaka kujitoa katika kundi la Wasafi kinaashiria kuwa amedhamiria kupambana mwenyewe.
Huo ndio ukweli kwa kuwa meneja wa kundi hilo, Sallam ameeleza kuwa msanii huyo ameandika barua ya kuomba kuvunja mkataba na kundi hilo.
Lakini kabla ya Sallam kubainisha jambo hilo jana Jumatano Agosti 21, 2019 katika mahojiano na televisheni ya Wasafi, Harmonize alikuwa ameanza kuonyesha dalili za kujiondoa katika kundi hilo.
Kwa sasa Harmonize anamiliki studio kubwa ya muziki iliyopo Sinza jijini Dar es Salaam.
Harmonize pia alijipanga kwa kuwa na lebo ya muziki ya Konde Gang ambayo inafanya kazi zake kama ilivyo Wasafi, si rahisi kuendelea kufanya kazi kwenye lebo nyingine ilihali anayo ya kwake.
Pia amekuwa akipata mialiko ya kazi zake binafsi badala ya kupitia lebo ya Wasafi.
Habari zinazohusiana na hii
- Sababu Harmonize kutoonekana Wasafi Festival zaanikwa, aomba kuvunja mkataba
- Harmonize atakuwa msanii wa pili kuondoka Wasafi