Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Hizi hapa "Brand" zinazomilikiwa na Familia ya Kardashian

Kardashians Family Hizi hapa "Brands" zinazomilikiwa na Familia ya Kardashian

Sun, 18 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Familia maarufu kutoka nchini Marekani ‘Kardashian Family’ licha ya kupata umaarufu katika ‘Reality show’ yao lakini pia imepata mafanikio makubwa katika shughuli mbalimbali za ujasiriamali, huku biashara za Kim Kardashian zikipata mafanikio makubwa zaidi.

Katika familia hiyo wote ni watu wa kujishughulisha na pia ni watu ambao wanamiliki ‘Brand’ kubwa za vitu mbalimbali, tukianza na chapa maarufu ya ‘Skims’ inayomilikiwa na Kim Kardashian ilianzishwa mwaka 2009 na imekuwa na mafanikio makubwa ambayo inadaiwa kufikia zaidi ya dola 3.2 bilioni.

Ukiachilia mbali Kim kuna Kylie Jenner mwanadada anayemiliki vipodozi vya ‘Kylie Cosmetics’ vinadaiwa kifikia thamani ya zaidi ya dola milioni 600, vilevile kwa Kourtney Kardashian na chapa yake ya ‘Poosh’ yenye thamani ya dola 15 milioni.

‘Good American’ kutoka kwa #KhloeKardashian inayokadiriwa kuwa na thamani ya dola 12 milioni, yupo #KendallJenner na chapa yake ya ‘818 Tequila’ ambayo ilitambulishwa mwishoni mwa mwaka 2023 chapa ambayo bado haina mafanikio zaidi, huku wadau wakidai kuwa ni kutokana na mwanadada huyo kugoma kutumia jina la famila katika chapa hiyo.

Kris Jenner ambaye anamiliki chapa ya bidhaa za usafi za kusafishia mikono na vyombo iitwayo ‘Safely’ ambayo inapatikana katika mtandao wa Amazon inadodaiwa kuuzika sana nchini Marekani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live