Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hivi ndivyo gari la Timbulo lilivyoteketea kwa moto

Timbuloooo Timbulo

Sat, 18 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Gari aina ya IST mali ya Msanii wa Bongo Fleva, Ally Mohamed Timbulo @timbulo limeteketea kwa moto Ubungo Riverside Jijini Dar es salaam kutokana na kinachoaminika kuwa ni hitilafu ya umeme ya gari hilo.

Timbulo amesema hakuna yeyote aliyejeruhiwa kutokana na tukio hilo na yeye hakuwepo kwenye gari wakati huo ila tu ni hasara ya gari lenyewe lenye thamani ya milioni 14 ambalo hakuwa amelikatia BIMA kubwa.

"Gari lilikua na shoti ndani kwa ndani na inavyotokea matatizo kama hivi ndio Mtu unaona lazima wa kuwa na BIMA kubwa, unabaki unajutia tu ningekuwa na bima kubwa ningekua nalipwa gari jingine, Watu inabidi tujifunze BIMA ina umuhimu wake," amesema Timbulo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live