Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hivi ndivyo Profesa jay alivyokutana na mkewe siku ya kwanza

Prof Jay Rttrt Hivi ndivyo Profesa jay alivyokutana na mkewe siku ya kwanza

Thu, 30 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Grace Mgonjo, mke wa supastaa wa HipHop Bongo, Joseph Haule 'Professor Jay' amefunguka namna ambavyo walivyoweza kukutana na mume wake huyo kabla hawajawa wapenzi.

Ambapo kwa maelezo yake amesema kuwa yeye na Professor Jay walikutana American Chips maeneo ya Kinondoni ambapo alikuwa anaelekea field, alisimamishwa na baadae akaombwa namba ya simu lakini alipomuuliza jina akaambiwa anaitwa Joseph.

“Tulikutana American Chipsi Kinondoni, asubuhi nilikuwa nikienda kazini field, yeye sijui alikuwa anatokea wapi. Mimi nilikuwa simjui wala sijui kabisa maisha yake kama ni staa au mwanamuziki kwa sababu hata mimi hayakuwa maisha yangu ya mitandao.

“Akajitambulisha kwama ‘mimi ninaitwa Joseph’, akaomba namba yangu nikampa nikaondoka wala sikujali, sijui kama ni Profesa Jay najua ni Joseph tu nikatupa namba nikachukua yak wake nikaondoka zangu maisha yakaendelea.

“Alikuja kistaarabu alivyokuja kunisalimia ndiyo maana sikujali. Akakaa we ndiyo baadaye akaja kunitafuta baada kama ya wiki tatu ama mwezi. Labda alikuwa anajiuliza huyu mtu hanijui ama? Ndipo tukaanzia hapo.

“Ndiyo akaanza kuniomba twende kwenye shoo Morogoro, ndiyo nikajuamuuliza wewe ni nani akaniambia ni msanii, nikaanza kumfuatilia na kumjua. Hata akitaka kuonana na wewe alikuwa anakuomba date kistaraabu sio kihuni, mnatoka mnaenda sehemu mnakaa, mnazungumza, kuanzia hapo mahusiano yetu yakaanza,” amesema mke wa Prof. Jay.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live