Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hivi ndivyo Diamond, Wema walivyoanzisha penzi Facebook

9357 Pic+diamond TZW

Mon, 18 Jun 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

“Mimi na Diamond tuliwahi kukutana mara moja tu kipindi kile Billcanas na hatukuwahi kusalimiana kabla ya kuanza uhusiano lakini tulikuwa tunaangalianasana. Kwa hiyo nakumbuka alikuwa yupo ‘smoking room’ (chumba cha kuvutia sigara) kwa hiyo tukawa tumepeana migongo, mimi nilikuwa na rafiki zangu wawili

“Nikamuona akaniona yeye alikuwa na rafiki yake, hatujasalimiana hatujafanya chochote mimi nimechukua vinywaji tukatoka nje na marafiki zangu. (Wakati) tumesimama hapo nje nikawa naambiwa ‘yule ndio ameimba Kamwambie’. Kipindi hicho nilikuwa namuona wa ajabu sana ila tu ‘alijisekshisha’ kiasi fulani, mimi nilikuwa natoka na Chaz Baba so’ nakumbuka hiyo ndio ilikuwa mara ya kwanza kuonana.

“Mimi nikasafiri kwenda Marekani, nilipofika kipindi hicho Kamwambie ndio ilikuwa hot na wimbo wa Mbagala ndio kauachia. Dada zangu walikuwa wanampenda sana Diamond kutokana na nyimbo zake, dada yangu wa kwanza alikuwa anaona Bongo inafanya vizuri kimuziki, akaniuliza kama tuna urafiki na Diamond nikasema sio sana tunajuana tu. Akaniambia nimwambie aende Marekani kufanya shoo sababu kila party tuliyokuwa tunaenda lazima watapiga Kamwambie halafu kila mtu anaupenda.”

Wema anasema hapo ndipo watu wakaanza kumwambia atafute mawasiliano ili Diamond aende kufanya shoo Marekani.

“Nilimwambia Da Rehema (Ray C) anitafutie namba zake, siku moja nikaona Diamond ana mpango kwenda kufanya shoo London, nikamtumia meseji, nikamwambia ‘hey mambo vipi mzima upo London’ akaniambia ‘hapana mamie sipo London sijui ni nani’ nikamwambia Wema hapa nipo Marekani halafu una mashabiki wengi sana huku, akaniambia basi sawa acha nimalize ishu ya London halafu nitakuambia.

“Siku moja tukanuniana, alikuwa amealikwa Ikulu halafu nikawa namtumia meseji hajibu, nikimpigia simu hapokei akaja akatoka akanipigia simu nikawa sijibu. Akanitumia meseji ‘baby I’m sorry, wewe ndio faraja yangu sijui ni nini…. I LOVE YOU. Sikuona kitu kingine chochote nikaona tu hiyo. Basi nami nikamjibu sawa nimekusamehe lakini sijakusamehe sana, nimekusamehe kidogo.”

Wema akaendelea kusema, “mimi nilimwambia aniambie kitu kizuri na mimi nikamwambia I LOVE YOU. Basi akaniambia ‘mwenzio nakupenda, nachanganyikiwa’ basi hapo ndio mapenzi yakaanza, kwa hiyo niliporudi kutoka Marekani mimi na Naseeb tukaanza kuishi pamoja.”

Wema anasema yeye na Diamond wamekaa pamoja mwaka mzima kama mke na mume.

Kwa nini mliachana?

“Mimi na Diamond tuliachana baada ya yeye kunichiti na Jokate, nilikuwa sijui na maisha yangu yote tangia nimeanza mapenzi na Diamond kipindi hicho, kwani tulikuwa tunapendana sana hata kumfuatilia niliona nitayaharibu mapenzi yetu,” anasema nyota huyo wa filamu hapa nchini.

Chanzo: mwananchi.co.tz