Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Hivi ndivyo Danelo alovyotoroka gerezani

Daneloo (15).jpeg Hivi ndivyo Danelo alovyotoroka gerezani

Fri, 8 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msako wa Muuaji Danelo Cavalcante (34) unaendelea baada ya kutoroka katika gereza la Pennsylvania nchini Marekani wiki iliyopita kwa kutumia njia aliyotumia Mfungwa mwingine kutoroka miezi michache iliyopita ya kutembea kama Spider Man katikati ya kuta mbili.

Cavalcante ametoroka Gereza la Kaunti ya Chester Alhamisi ya wiki iliyopita ambapo video ya CCTV imeonesha jinsi alivyofanikiwa kutoroka.

Mlinzi wa Gereza, Holland, amesema Mfungwa huyo hakuonekana na Mlinzi yeyote wakati akitoroka na hata waliokuwa wakifuatilia camera za CCTV kwenye chumba maalum hawakumuona ambapo Walinzi wote wa zamu wa siku hiyo waliokuwa mnarani wamepewa likizo ya kiutawala na wanachunguzwa kwa uzembe.

Cavalcante alipatikana na hatia ya kesi ya mauaji ya daraja la kwanza August 16 baada ya kumuua EX wake, Deborah Brandão mwenye umri wa miaka 33, mwaka 2021, alihukumiwa kifungo cha maisha bila msamaha pia anasakwa katika kesi ya mauaji ya 2017 huko Brazil ikiwa ndio Nchi yake ya asili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live