Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hivi Wema aliamua au alishauriwa kujikondesha?

WEMA SASA NA ZAMANI Hivi Wema aliamua au alishauriwa kujikondesha?

Fri, 5 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mimi ni shabiki tu kama mashabiki wengine wa kiwanda cha filamu na burudani kwa ujumla. Namfahamu muigizaji Wema Sepetu kitambo kidogo, tangu aliposhinda lile shindano la Miss Tanzania mwaka 2006.

Namfahamu Wema ambaye alikuwa na mwili fulani wa saizi ya kati wakati anaanza kuigiza, baada ya kipaji chake kuonekana na aliyekuwa nguli wa sinema za Kibongo, marehemu Steven Charles Kanumba.

Wema wa Kanumba alikuwa na mwili uleule niliokuwa nautaka mimi. Mwili ambao ukishika mkono unaona yes huu ni mkono. Umaarufu aliokuwa nao kwenye umiss uliongezeka maradufu baada ya kuanza kuigiza na kasauti fulani hivi ka upole.

Unaweza kusema Wema naye alikuwa na mchango wa mafanikio ya Kanumba. Kanumba aliongezeka thamani hasa baada ya kuwa karibu kikazi na hata kimahusiano.

Mafanikio ya umaarufu yalimuongezea kidogo mwili zaidi Wema. Akapata ule mwili wa kuelekea kwenye ukibonge fulani hivi. Hii ilinifanya mimi na mashabiki wengi wa Wema kuzidi kumpenda na jinja lake lilizidi kukua. Wema alimfanya hata Diamond awe maarufu zaidi. Ana kismati fulani hivi. Uzuri hata moyo wake ni wa kusaidia bila kujali malipo. Alijitoa kwa Diamond, waliongezeana umaarufu na kapo yao ilikuwa miongoni mwa kapo bora zaidi kuwahi kutokea Bongo. Wema alikuwa akikatiza mahali, kunakuwa na mshtuko fulani kwamba amepita mahali hapo. Yani hata kama utakuwa na roho mbaya lakini lazima utaguswa kumtazama maana jina lake lilikuwa kubwa lakini muonekano wake ulikuwa unamfanya awe wa kipekee. Alikuwa amegawanyika vizuri, muonekano wa kibantu ambao ulikuwa unakubali kila aina ya nguo. Akivaa gauni sawa, akivaa suruali pia bado mambo yalikuwa mwake mwake. Huu ulikuwa wakati wake kulamba madili kibao ya ubalozi.

Hata alipoachana na Diamond, haikumfanya yeye aendelee kupendwa. Alikuwa tayari na kijiji chake na hap ahata baadhi ya watu walisema huwenda Diamond anaweza kusuasua kwenye kukuza jina lake baada ya kuachana.

Miaka kadhaa iliyopita, Wema aliamua kujikondesha. Sijui aliashauriwa na nani. Sijui ni mawazo yake yeye mwenyewe au watu wake wa karibu au vipi. Alikuwa anataka kukonda hivi alivyo sasa ili iweje? Mbona ule muonekano wake wa zamani ulishamtengenezea stardard fulani nzuri kwa mashabiki wake?

Mbona kama ameamua kuwapoteza mashabiki waliokuwa wanamkubali akiwa na mwili ule? Mbona mwili ule haukuwa mnene wa kupitiliza? Nimeangalia picha za juzikati alipokuwa Mtwara kwenye kuhamasisha chanjo, nikasema kwa nini jamani?

Kwa nini Wema aliamua kujikondesha? Yale ni maamuzi yake lakini daah kwa kweli sisi mashabiki wake hatujapenda. Kama inawezekana, rudi tu kule ulipokuwa bhana. Mimi Kidau, shabiki wa wema!

Chanzo: www.tanzaniaweb.live