Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hii ndo sababu ya Harmonize kufuta tattoo ya Diamond

Sd Harmo Gl Hii ndo sababu ya Harmonize kufuta tattoo ya Diamond

Mon, 6 Nov 2023 Chanzo: Hii ndo sababu ya Harmonize kufuta tattoo ya Diamond

Staa wa Bongo, Rajab Abdul Kahali almaarufu Harmonize asimulia kufuta tattoo ya aliyekuwa bosi wake Diamond Platnumz.

Harmonize hapo awali alikuwa na tattoo ya aliyekuwa bosi Diamond yenye mchoro na maadishi "Simba"mkononi mwake.

Baada ya wanablogu kutaka kujua iwapo msanii huyu bado amehifadhi tattoo ya Diamond kwenye mkono wake aliwaonesha sehemu ya ngumi kwenye mkono wake kuashiria tayari alikuwa amefuta Tattoo hiyo.

Kwenye mahojiano haya ya moja kwa moja na wanablogu wa mitandao , bosi huyu wa Konde Music Worldwide alisema kuwa yeye huchora tattoo kwa anayependa wakati ampamo anakerwa na uchukua hatua ya kufuta tattoo.

"Mimi huchora tattoo kwa upendo wa roho yangu mtu yeyote ninayempenda mimi huchora tattoo ila ninapokerwa na yeyote niliye na tattoo yake mimi huchukua jukumu la kuifuta na kuisahau,"alisema.

Harmonize hata hivyo alisimulia kuwa kuchora Tattoo kwa kabila lao la Makonde ni jambo la kawaida akisema kuwa bibiye yuko na tattoo usoni.

"Kuchora tattoo si jambo kubwa kwetu mimi mwenye nina tattoo mingi mpaka sijui hesabu zake kwa kabila yetu ya Makonde ni jambo la kawaida,"alisema.

Chanzo: Hii ndo sababu ya Harmonize kufuta tattoo ya Diamond