Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hii ndiyo 'six pack' ya Kiba inayomvuruga Maua Sama

Alikiba Maua Samma Hii ndiyo 'six pack' ya Kiba inayomvuruga Maua Sama

Thu, 29 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Maua Sama, msanii wa kike wa Bongo Fleva ameonyesha mahaba yake wazi wazi kwa bosi wa lebo ya Kings Music, Alikiba.

Sama akizungumza na wanablogu, alitetea hatua yake ya kutumia picha ya Alikiba kwenye utambulisho wa ukurasa wake wa Instagram, na kusema kwamba kando na kufukuzia kiki kwa ajili ya ngoma yake mpya, pia anampenda Alikiba kutoka ndani ya moyo wake.

Alimtaja Alikiba kama msanii ambaye ana moyo mweupe sana katika suala zima la kutoa sapoti kwa msanii yeyote.

Kando na hilo, Sama pia alisema kwamba mwili wa sixpack wa Alikiba unamnyima usingizi kila mara anapoona picha zake, jambo lililomchochea kuitumia moja ya picha zake kama DP ya Instagram.

“Nampenda Alikiba, kusema kweli na pia kwenye suala zima la... si unajua umetoa nyimbo lazima utengeneze upepo. Hamna shida katka hilo. Lakini pia nampenda Alikiba kutoa mfunguni mwa moyo wangu kwa sababu yeye ni msanii ambaye ako vizuri na pia wakati inakuja kwa kukupa sapotim anafanya hivyo 100%,” Sama alisema.

“Lakini pia ana mwili mzuri sana, lakini yeye kwangu ni kama kakangu. Na mimi kama dadake ninakubali sana jinsi mwili wake unavyomtoa. Sijawahi mwambia hivyo kwa sababu namchukulia kama kaka yangu,” aliongeza.

Mrembo huyo ambaye amekuja na wimbo mpya baada ya mwaka wa 2023 wenye changamoto nyingi upande wake alisema kwamba aliathirika pakubwa kisaikolojia baada ya kuharibikiwa na mimba.

Mkali huyo wa ‘Iokote’ alisema kwamba mwaka jana aliharibikiwa na mimba na ni jambo ambalo mpaka leo hii hapendi kabisa kulizungumzia kwa sababu linamuumiza sana na kumkumbusha machungu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live