Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hii ndio sababu Davido kutoshirikisha wabongo

Davido Md.jpeg Davido

Tue, 18 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii Davido ambaye anazidi kutamba na kutambaa kwa kasi na ngoma zaidi ya 15 kwenye albamu yake mpya ya ‘Timeless’ kwa mara ya kwanza amefunguka ni kwa nini hakumshirikisha msanii yeyote kutoka Tanzania katika albamu hiyo.

Akizungumza na Amazon Music katika podcast ya +44 kama moja ya mahojiano anayoendelea kufanya kuisukuma zaidi albamu yake, alisema kuwa anaogopa sana kufanya muziki na msanii halafu mashabiki wa msanii pinzani kwa huyo msanii waanze kumshambulia.

“Nikienda Tanzania kwa mfano na nifanye Kolabo na msanii huko, halafu nirudi nyumbani nianze kuona komenti za kejeli na matusi pengine msanii huyo ana mpinzani na mashabiki wa mpinzani wake wamechizi kwamba nilikwenda huko... unajua kitu kama hicho kitakubadilisha kabisa jinsi ulivyokuwa unawaza,” Davido alsiema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live