Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Hii ndio mitindo ya nywele inayokubaliwa na Serikali ya Korea

Nywele Korea Hii ndio mitindo ya nywele inayokubaliwa na Serikali ya Korea

Mon, 12 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nchini Korea Kaskazini (DPRK) kuna sheria iliyoidhinishwa na serikali inayoelekeza aina ya mitindo ya nywele kwa wanawake na wanaume wa nchi hiyo.

Gazeti la Daily Mail la uingereza liliwahi kuripoti kwenye makala yake mwaka 2017 likisema katika nchi hiyo wanawake wameruhusiwa kuchagua mitindo 15 iliyoidhinishwa na serikali, ambapo wanawake walioolewa wanatakiwa kuwa na nywele fupi na wale ambao hawajaolewa wameelekezwa kuwa nywele ndefu, zilizomwagika na zilizojisokota.

Wanaume pia wana mitindo yao 15 iliyoidhinishwa na serikali ambapo wao ni marufuku kufuga nywele zaidi ya sentimita 5, isipokuwa kwa wazee/watu wazima ambao wao wana kibali cha kufuga nywele kwa urefu usiozidi sentimita 7 (nchi 3).

Inaelezwa kuwa sheria hii imeleta usawa katika mitindo ya nywele baina ya wanawake na wanaume nchini Korea.

Mwaka 2005 gazeti la Daily Mail liliwahi kuripoti kuwa televisheni ya Taifa ya Korea iliandaa vipindi maalumu vya muendelezo (series) vinavyoelekeza namna ya ukataji wa nywele na mitindo mbalimbali ya ukataji nywele kwa style ya kisasa ya kijamaa.

Katika aina hizo za mitindo ya nywele kuna aina mbili za unyoaji ambazo zimewekwa kwa kundi maalumu.

Katika mitindo hiyo kuna mtindo maalumu wa nywele ambao unanyolewa na kingozi wao nchi hiyo tu, Mwenyekiti Kim Jong Un na kuna mitindo kwa ajili wanajeshi, walimu, wanafunzi na kundi maalumu la viongozi n.k.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live