Usiku wa Tuzo za Grammys huwa sio kwa ajili tu ya kuwapa Tuzo wale waliofanya vizuri kwenye Muziki, bali pia ni sehemu ya kutazama mastaa wanaojua kuvunja kabati na kuvaa vitu vya gharama.
Hapa leo tumewekea orodha ya mastaa wa Kiume ambao walivaa Saa kali na za gharama kwenye mtoko wa Tuzo hizo za 65.
Jay-Z alitupia mkononi saa aina ya Patek Philippe (Grandmaster Chime) yenye thamani ya USD 2.2M sawa na zaidi ya TSh. BILIONI 5.
Pharrell Williams alitupia saa aina ya Richard Mille (RM 88 Automatic Tourbillon Smiley yenye thamani ya USD 3M sawa na zaidi ya TSh. BILIONI 7.
Dwayne Johnson au The Rock mkononi aliweka kidonda aina ya Panerai (Radiomir PAM00515) yenye thamani ya USD 21K sawa na zaidi ya TSh. MILIONI 50.
Kendrick Lamar alitupia Rolex (Perpetual Oystersteel 41) yenye thamani ya USD $25,000 sawa na MILIONI 58 za Kitanzania. Lil Uzi Vert aliweka Richard Mille yenye thamani ya USD 400k sawa na TSh. MILIONI 935. DJ Khaled alicheza na Rolex pia macho ya Tiger yenye thamani ya USD 215k sawa na zaidi ya TSh. MILIONI 500