Ngoma mpya ya Diamond Platnumz, Komasava imeendelea kuteka mioyo ya mashabiki dunia na sasa supastaa wa Marekani, Chris Brown ameonekana akicheza wimbo huo kupitia mtandao wa TikTok.
Hata hivyo, mtayarishaji wa ngoma hiyo Salmin Maengo ‘S2KIZZY’ ameeleza kuwa wimbo huo ambao Diamond amemshirikisha Chley na Khalil Harrison umerekodiwa wakati wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani tena ndani ya dakika sita kila kitu kilikuwa kimemalizika.
“I’m speechless on this one … @chrisbrownofficial #komasava certified global anthemworldwide hit @diamondplatnumz this is big for the culture and for africa we move now … Oya wanangu ni @chrisbrownofficial kwenye beat ya zombieeeeee put some respect on my name forever.
“NB; this song was made on 27 day of Ramadhan ???? Diamond recorded his part only in 6 minutes god is good allahu albar” S2KIZZ ameandika kupitia ukurasa wake wa Instagram.
Hii si mara ya kwanza Chris Brown kuvutiwa na wasanii wa Afrika wiki iliyopita kwenye ziara yake ya ‘11:11’ alitumbuiza na kucheza ngoma ya ‘Tshwala Bam’ iliyoimbwa na mwanamuziki kutoka Afrika Kusini, Titom aliyomshirikisha Yuppe.
Wimbo wa ‘Komasava’ (Comment Ça Va) unaendelea kupasua anga duniani kutokana na lugha kadhaa kutumika ndani yake.
Kabla ya Chris Brown kufanya Challenge hiyo mtandaoni, mastaa kibao wakiwemo wanasoka wamewahi kufanya pia na kuweka kwenye kurasa zao za mitandao ya kijamii akiwemo Swae Lee kutokea kundi la Rae Sremmurd, Maitre Gims kutokea Ufaransa, Paul Pogba na wengine kibao.
Kwa sasa mtandao wa Tiktok umekuwa ukiwabeba mastaa wakubwa wa muziki duniani kwa kupaisha ngoma kupitia challenge. Kwa Diamond ukiachana na Komasava, ngoma nyingine Mavokali wa Commando ambao ulitazamwa kwa kasi kufikisha watazamaji milioni 22 kwenye mtandao wa YouTube.
Kwa sasa ni kama Chris Brown ameuongezea mwendo ngoma hiyo kwani, ndani ya saa chache tangu ameposti video kwenye Tiktok, Komasava imeshafikisha watazamaji milioni 2.7 ndani ya mwezi mmoja.
Mastaa zaidi waucheza
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Breezy ameonekana akicheza ngoma ya ‘Komasava’.
Jaymelody yeye ameandika: “Sema mwana itabidi apostiwe ampaka aone eeh kayakanyaga, Hongera sana brother Diamond”
Huko kwa D Voice naye hakuna dogo unaambiwa kwani naye kashauri jina la Diamond liandikwe kwenye vitabu vya historia.
“Heshima unaloipa hili Taifa kiukweli ni kubwa sana, tumezoea kuona viongozi wa nchi tu wakipewa heshima zinazostahili kulingana na waliyoyatenda katika uongozi wao nadhani unastahili heshima hiyo.
Barnaba naye amemwaga maua kwa Mondi pamoja na S2kizzy ‘Zombie’ kwa kuendelea kupeperusha bendera ya Tanzania kimataifa.
“Congratulations champion @diamondplatnumz unaweza kuona ni jambo dogo sio dogo hata kidogo sasa bendera imepeperuka vyema to big @diamondplatnumz & @s2kizzy zombie chapa tena brizzzzz si huyu hapa Comasava to the world”.