Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hii hapa siri nzito usiyoijua kuhusu Joti

Joti Pic Data Msanii Joti

Sun, 15 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Unaweza kudhani mwonekano wa mwili wa mchekeshaji maarufu, Lucas Mhuvile ’Joti’ uko tu vile ulivyo, lakini ukweli ni kwamba utakuwa unajidanganya kwani jamaa anaufanyia kazi kubwa ili kuendelea kudumu kwenye sanaa.

Akizungumza nasi, Joti alisema amekuwa akijitahidi kufanya mazoezi na kupangilia kula vyakula ili kuepuka kuongezeka mwili sababu kubwa ikiwa kujiweka tayari kuigiza nafasi zote ambazo amekuwa akizicheza.

Joti ni mmoja wa wasanii wenye vipaji, ambaye anaweza kuigiza nafasi tofauti kuanzia ile ya mtoto wa kike na wa kiume, dada, kaka, baba, mama, babu hadi bibi.

“Hizi nafasi ninazocheza ambazo ndiyo zinazoniweka sokoni hadi leo, zinanifanya niufanyie kazi sana mwili wangu kuanzia kwenye kula hadi mazoezi, kwakuwa nikijiachia sana sitaweza kuzimudu.

“Ukweli ni kwamba nikisema nijiachie, mwili wangu sio huu mnaouna, lakini kwa kuwa sanaa ndio kazi inayoniweka mjini, inabidi nijitahidi nisiwakwaze mashabiki wangu na kuendelea kuwapa kile wanachonipendea,” alisema Joti mwenye majina mengi ya kisanii ikiwemo Andunje, Dada Kiboga na sasa akitesa zaidi na jina la Nishai.

Joti aliyeanza kupata jina akiwa na kundi la Nyota Assemble, alipata jina zaidi akiwa kundi la Original Comedy likiwa na wasanii wengine akiwamo Wakuvwanga, MacReagan, Masanja na Vengu.

Hata hivyo, baada ya kusambaratika, Joti ameonekana kuendeleza moto wake katika tasnia ya uchekeshaji na katika tuzo za filamu mwaka juzi aliibuka kidedea katika kipengele cha mchekeshaji bora lakini mwaka huu bahati haikuwa yake, kwani ushindi huo umeenda kwa Mkojani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live