Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hereni zangu zitanunua jeneza siku nikifa - Morgan

Earring Morgan Hereni zangu zitanunua jeneza siku nikifa - Morgan

Fri, 10 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Muigizaji mkongwe wa filamu Morgan Freeman afichua siri ya hereni zake za dhahabu alizo zivaa kwa miaka mingi.

Kupitia Mtandao wa Kijamii wa Instagram Freeman amemjibu Shabiki kwa Kumuambia kuwa, siku akifa, hereni hizo ndizo zitatumika kumununulia jeneza kwa ajili ya maziko yake.

“Nimekua nikiulizwa kuhusu hereni hizi kila wakati, ukweli ni kwamba, hereni hizi zina thamani ya kutosha kwa mtu kuninunulia jeneza ikiwa nitakufa ugenini. Ndio maana mabaharia walikuwa wanavaa na ndio maana navaa,” amesema Morgan.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live