Duniani kumekuwa na aina nyingi za magari, na kila mtu huwa na chaguo lake, japo yapo yale ambayo yakionekekana barabarani watu hujiuliza litakuwa linamilikiwa na nani kutokana na gharama zake.
Gharama za magari hayo mara nyingi hutofautiana kutokana na ubora, na muonekano wake. Fahamu aina tano za magari yenye gharama kubwa zaidi duniani.
Gari aina ya Rolls Royce Boat Tail, linaongoza kuwa gari la thamani zaidi duniani bei yake ni dola 28 milioni ambayo ni zaidi ya tsh 70.2 bilioni, likifuatiwa na Bugatti La Voiture Noire la $18.6 milioni ni zaidi ya tsh 46.6 bilioni.
La tatu ni Pagani Zonda HP Barchetta $17.5 milioni sawa na tsh 42.6 bilioni,linafuata SP Automotive Chaos $14.4 sawa na tsh 36.1 bilioni, namba tano inashikiliwa na Rolls Royce Sweptail $13.2 milioni ni zaidi ya tsh 33.1 bilioni.