Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Haya ndio madhara ya kutazama Filamu za kutisha kwa watoto

Legacy Horror Haya ndio madhara ya kutazama Filamu za kutisha kwa watoto

Sun, 15 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wiki iliyopita zilisambaa taarifa za kifo cha mtoto wa miaka 12, mkazi wa Same mkoani Kilimanjaro aliyejinyonga wakati akifanya maigizo baada ya kutazama filamu za kuogofya.

Taarifa zinaeleza kuwa, mtoto huyo aliyekuwa akiishi na bibi yake mlezi, alitazama filamu ya kutisha kisha asubuhi akataka kuigiza kujinyonga kwa kutumia shuka kama alivyoona kwenye filamu, akiamini hatakufa, lakini kwa bahati mbaya akafariki dunia.

Kisa hiki ni moja ya ushahidi kuwa, wazazi wanapasawa kuwa macho katika kuwaongoza watoto wao juu ya maudhui ya kutazama sambamba na kuwapangia muda maalumu wa kutazama runinga.

Inaelezwa kwa kawaida muda wa mtoto kuangalia runinga siku za kawaida hauzidi saa moja au saa tatu kwa mwisho wa juma.

Kwa mujibu wa Taasisi ya Kitaifa ya Afya ya Akili (NIMH) ya Marekani, utafiti uliofanywa ukihusisha ‘athari za sinema za kutisha kwa watoto’ zinazoweza kuwa na athari za muda mrefu zisizopendeza kwa watoto, unaonyesha zinaweza kusababisha wasiwasi kwa watoto, ikiwamo shida ya kulala, uchokozi na kujihatarisha.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live