Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hawa ‘Nitarejea’ wa Diamond aibuka upya

70174 Hawa+oic

Tue, 6 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Msanii wa Bongo Fleva, Hawa Said maarufu kama Hawa Nitarejea ametoa wimbo wa ‘Nacheka’ baada ya kupona maradhi yaliyokuwa yanamsumbua kwa muda mrefu.

Hawa ambaye amewahi kutamba na wimbo wa ‘Nitarejea’ alioshirikishwa na mwanamuziki Diamond Platnumz amesema, “Nimetoa wimbo ‘Nacheka’ ikiwa ni zawadi kwa mashabiki wangu.”

“Lakini ni shukurani kwa Diamond na kundi zima la Wasafi ambao kwa ushirikiano wao walifanikisha kunipeleka nchini India kutibiwa maradhi ya moyo na sasa nimepona ninamshukuru Mungu.”

Akizungumza na Mwananchi, Hawa amesema ametoa wimbo huo pamoja na video yake kwa sababu anataka mashabiki wake mbali ya kusikia sauti wamuone alivyopona na kuwa na siha njema.

“Watanzania ninaamini waliniombea, nimetoa wimbo huo na video ili waone maombi yao yalivyozaa matunda, nimepona na ninaimba, ”amesema.

Amesema mashabiki wake wakae mkao wa kula kwa maelezo kuwa wimbo wa Nacheka ni mwanzo wa burudani nzuri zitakazokuja kutoka kwake.

Pia Soma

Chanzo: mwananchi.co.tz