Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hawa Nitarejea ajifungua, amshukuru Diamond

Hawa Ntarejea Hawa Nitarejea ajifungua, amshukuru Diamond

Wed, 6 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanamuziki Hawa Nitarejea ameonesha furaha yake ya kupata mtoto wa kike huku akimshukuru Diamond kwa kumsaidia katika kila hali.

Kupitia ukurasa wa Instagram wa mwanadada huyo ameshusha ujumbe ukieleza;

“Alhamdulillah napata muda wa kushukuru, nimekumbuka nilikotoka haikuwa rahisi na sikuwaza mwanzo kama nitaitwa tena mama, Ila Diamond Platnumz Mungu akubariki sana akuzidishie palipopungua mashaallah una moyo ambao sijui kuufananisha katika maisha yangu ulinikomboa pakubwa Alhamdulillah, sio tena Nasibu nimepata binti anaitwa Mariam.

Alhamdulillah, nawashukuru watanzania wote kwa upendo wenu wa hali na mali kwangu nguvu zenu ni kubwa nawapenda sana Mungu awabariki in shaa allah.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live