Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hatuwezi kupokea tuzo za Harmonize Airport

Capture 564?fit=483%2C242 Hatuwezi kupokea tuzo za Harmonize Airport

Thu, 16 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanamuziki Baba Levo amesema tuzo alizopata Harmonize ni tuzo ndogo ambazo hazina hadhi ya kwenda kupokelewa Airport.

Wikendi iliyopita ulikuwa ni wakati wa kihistoria na wa kukumbukwa milele katika maisha ya kimuziki ya msanii Harmonize baada ya kushinda tuzo 3 kwa mpigo katika hafla iliyoandaliwa nchini Marekani.

Harmonize alishinda tuzo 3 kwa kuwabwaga wasanii wakubwa wa Afrika katika tuzo za African Entertainment Awards.

Tuzo ya kwanza aliyoshinda kwa kura nyingi ni tuzo ya msanii bora wa mwaka barani Afrika, akashinda pia video bora ya mwaka kupitia ngoma yake ya Single Again na pia akatajwa kama mfalme wa muziki wa Afrika Mashariki na Bongo Fleva kwa jumla.

"Hatuwezi kwenda Airport kupokea utoto sisi siwezi kuongea sana sababu hizo ni biashara za watu wewe umeona nani kaposti hizo tuzo zaidi ya Harmonize mwenyewe?

"Hizo ni tuzo ndogo sana hazina hadhi hata ya kwenda kupokelewa airport. Harmonize ninakutana naye cassino na maeneo mengine, tunasalimiana ananipa laki tano, ananikubali mimi ndugu yake," amesema Baba Levo.

Katika tuzo hizo, Harmonize aliwaonyesha kivumbi wasanii kama vile Libianca kutoka Cameroon ambaye amekuwa akifanya vizuri, Asake, Burna Boy, Davido, Tiwa Savage, Yemi Alade, Rema wote kutoka Nigeria lakini pia Diamond Platnumz kutoka nyumbani Tanzania.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live