Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hatimaye kitumbo cha Nandy hadharani

Nandy Ujauzito Hatimaye kitumbo cha Nandy hadharani

Thu, 7 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya tetesi kuzagaa kwa muda mrefu huku mwenyewe Nandy akiwa anachengachenga kuhusu suala la ujauzito, hatimaye mumewe mtarajiwa, Billnass ameanika kitumbo chake.

Billnass ameanika picha hiyo jana Julai 6, 2022 kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo aliweka picha yake akiwa amesimama na Nandy lakini haonekani sura lakini tumbo likionekana live ni mjamzito.

Kwenye picha hiyo hakuweka maneno mengi zaidi ya kuandika; “JESHI YA @Nengatronix” Kilichofuata hapo ni pongezi kutoka kwa kwa mastaa na mashabiki mbalimbali wa kapo hiyo ambayo inapendwa sana mitandaoni.

Zipo taarifa zinadai kuwa tayari Nandy ameshajifungua na ndio sababu iliyochelewesha harusi yao japo wenyewe hawajaweka wazi. Tanzaniaweb.com inawatakia kila lakheri Nandy na Billnass.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live