Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hatimaye Zari atangaza kufunga ndoa

Zari 7 Hatimaye Zari atangaza kufunga ndoa

Tue, 20 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ni wazi kuwa mwanasoshalaiti Zari Hassan anayafurahia sana mahusiano yake mapya na hivi karibuni huenda tukashuhudia akifunga ndoa kibenten wake.

Mzazi mwenza huyo na msanii Diamond Platnumz amedokeza kufunga pingu za maisha na Shakib Cham Lutaaya baada ya kufichua kuwa mpenzi huyo wake wa sasa anapanga kupeleka posa kwa baba yake nchini Uganda.

"Shakib aliniambia jana kuwa anataka kukutana na baba yangu. Anataka kutoa posa kwa ajili ya ndoa, yuko tayari kunioa," alisema Zari kwa Kiganda katika video ambayo ilipakiwa kwenye mtandao wa Snapchat.

Katika video hiyo fupi, mama huyo wa watoto watano aliendelea kuwatupia vijembe wakosoaji wa mahusiano yake na Shakib huku akiwathibitishia kuwa juhudi zao kuwatenganisha zilikuwa zimefeli.

"Waliosema itaishia kwa machozi rudini kwa waganga wenu mkaombe warudishe hela, uchawi haukufanya kazi," alisema.

Hivi majuzi Zari alibainisha kuwa mpenzi wake mpya anampa amani ambayo imemwezesha kukua na kung'aa zaidi.

"Naanza kuwa mkubwa. Naona shavu. Nimejipa amani sana. Bwana Lutaaya unanipa amani sana kwa maana, watu, ngojeni niwaambie kuhusu amani ya akili, hiyo nawaambia hata ufanye nini, unakua mkubwa zaidi hata usipokula," alisema kupitia Tiktok.

Mwanasoshalaiti huyo alimtaka Shakib kuendelea kumpatia mahaba anayompa na kumbainishia kuwa yanafanya kazi.

" Lutaaya chochote unachofanya, ongeza zaidi. Niongezee dozi nyingine, chochote unachofanya kwa sababu zinafanya kazi, zinafanya kazi. Hata hao wanaoroga wamekata tamaa, wanahitaji kurejeshewa pesa zao. Bado nina amani, nendeni mkaombe kurejeshewe pesa zenu," alisema Zari.

Zari amekuwa akitetea mahusiano yake na Lutaaya hasa kwa kuwa amekosolewa sana kufuatia utofauti wao wa kiumri. Wiki chache zilizopita alifichua kuwa amempiku mpenzi huyo wake kwa takriban miaka kumi.

"Mpenzi wangu sio mdogo. Ana miaka 30 anaelekea 31 Desemba mwaka huu. Yeye sio mdogo, anaonekana mdogo. Mimi natimiza miaka 42 mwaka huu na huwezi kujua," alisema Zari.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live