Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hatimaye Dimpoz afunguka siri nzito ya kutokuwa na mabaunsa

Ommy Dimpoz Nn.png Dimpoz

Sat, 14 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii maarufu wa Bongo Fleva, Ommy Dimpoz amesema kuwa hawezi kutembea akiwa na mabaunsa kama wanavyofanya wasanii na watu wengine maarufu nchini.

Kupitia Kipindi cha Leo Tena kinachoruka kupitia Clouds FM, Dimpoz amesema;

“Mimi sina mabaunsa na siwezi kulaumu watu wanaotembea na mabaunsa, mimi nije na mabaunsa hapa studio kwani nyie mnapiga watu, labda niende kwenye event ambayo najua itakuwa na vurugu ndiyo naweza kwenda na mabaunsa.

"Naamini kuna sehemu za kwenda na mabaunsa na kuna sehemu za kwenda mwenyewe. Kuna wasanii unakuta ngoma zao hazijafika hata Kibaha na wanataka mabaunsa saba badala ya kupambana muziki wao ufike mbali”.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live