Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hatimaye Diamond, Harmonize uso kwa uso!

Diamond Harmonize Dsf Diamond na Harmonize

Tue, 6 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mastaa wa Bongofleva, Diamond Platnumz na Harmonize ni miongoni mwa watakaohudhuria uzinduzi wa albamu mpya ya Jux ‘King of Hearts’ utakaofanyika Desemba 7 mwaka huu katika ukumbi wa The Super Dome, Masaki.

Hii ni albamu ya pili kwa Jux baada kuachia ‘The Love Album’, (2019) yenye ngoma 18 ambayo Diamond alishirikishwa katika wimbo 'Sugua' uliofanya vizuri.

Ikiwa wote watafika kama alivyotangaza Jux, basi hili litakuwa ni tukio la kwanza la burudani kuwakutanisha Diamond na Harmonize ambao kwa sasa ni mahasimu wakubwa kimuziki.

Wiki mbili zilizopita wawili hao walitarajia kukutana katika jukwaa la Artist Master Class lililoandaliwa na Mziiki kujadili biashara ya muziki Tanzania, lakini Harmonize aliingia ukumbini baada ya Diamond kuondoka.

Diamond na Harmonize hawajawa na wakati mzuri wa maelewano tangu Harmonize alipoondoka kwenye lebo ya WCB Wasafi yake Diamond ambayyo ilimtoa kimuziki mwaka 2015.

Jux na Diamond wana ukaribu mkubwa wa kikazi na hata albamu hii ambayo imetoka tangu Novemba 25 ikiwa na nyimbo 16, wasanii wawili wa WCB, Zuchu na Mbosso wameshirikishwa.

Hata hivyo, ni tofauti kidogo na inavyoonekana kwa nje upande wa Harmonize, mapema mwaka huu Jux alieleza kushangazwa na kitendo cha Konde Music, Lebo yake Harmonize kutangaza atakuwepo kwenye shoo ya msanii huyo, Afro East Carnival.

Jux alisema Konde Music hawakuwasiliana naye wala menejimenti yake na kusisitiza hata kama ni kusaidiana kama wasanii lazima kuwe na mawasiliano ya pande zote mbili.

Katika hatua nyingine, Ben Pol amelalamika kuhusu kitendo cha Jux kuchapisha mabango mtandaoni kuwa atakuwepo katika shoo hiyo kwa madai hakuna makubaliano yoyote kati yao.

"Una namba yangu umeshindwa kunipigia au kunitumia ujumbe?, au watu wako kuwasiliana na watu wangu?, tunakuja kuona kwenye mitandao kwamba nitakuwepo kwenye show yako,".

"Wewe ulikasirika kwa Harmonize kukuweka kwenye matangazo ya event yake bila kukutaarifu au kukualika, ukafanya hadi interviews lakini na wewe unafanya kitu kilele. Napenda sapoti lakini hii ni style gani kaka" ameandika Ben Pol kwenye mitandao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live