Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hatimaye Baby Madaha aolewa!

Baby Madaha Hatimaye Baby Madaha aolewa!

Mon, 21 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kama kulikuwa na warembo ambao suala la mahusiano lilikuwa siri alikuwa ni Baby Madaha, kwa muda mrefu watu walikuwa hawamjui mwenza wake na hatimaye sasa, amemuanika baada ya kufunga ndoa.

Baby amefunga ndoa hiyo Novemba 19, 2022 ambapo kupitia ukurasa wake wa Instagram, ameposti picha mbalimbali za shughuli hiyo ambayo hakueleza umefanyikia wapi lakini ameweka picha za kanisani pamoja na ukumbini huku akisema amefunga ndoa kwenye siku yake ya kuzaliwa.

"I'm blessed indeed on 19th November = birthday& wedding day...wow!!" ameandika Baby Madaha.

Baby ni msanii wa muda mrefu ndani ya kilinge cha Bongo Fleva na amejipatia umaarufu zaidi kupitia ngoma yake ya mwanzoni kabisa inayokwenda kwa jina la Amore.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live