Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Hatari inayomkabili Oscar Pistorius akiachiwa leo

Pp Pistorius 2 Getty Oscar Pistorius

Fri, 5 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

 Ulimwengu wa wapenda michezo baadaye leo utashuhudia tukio la kuachiwa huru kutoka gerezani mwanariadha wa zamani wa mbio fupi, Oscar Pistorious, raia wa Afrika Kusini.

Nyota huyu anaachiwa huru baada ya kutumikia kifungo kwa miaka isiyopungua tisa, na sasa ataenda kutumikia kifungo cha nje hadi mwaka 2029.

Oscar (37), alihukumiwa kifungo cha miaka 13 jela baada ya kupatikana na hatia ya kumuua mpenzi wake, Reeva Steenkamp kwa kumpiga risasi mara nne.

Wakati akitenda kosa hilo siku ya Valentine mwaka 2013, Oscar alikuwa kwenye nyakati zake bora, ikiwa imepita mwaka mmoja tangu aende jijini London, England kushiriki mashindano ya ‘London 2012 on carbon fibre blades’.

Oscar alifanya tukio hilo kwa kutumia bastola akiwa nyumbani kwake Pretoria, nchini Afrika Kusini.

Alimuua Reeva aliyekuwa ameingia ndani ya nyumba hiyo wakati Oscar akiwa bafuni. Katika utetezi wake, nyota huyo alisema alifyatua risasi ikiwa ni sehemu ya kujihami kwani alijua mwizi ameingia nyumbani kwake.

Mbali ya kuachiwa kwa mujibu wa taarifa kutoka tovuti ya Dail Maily zinadai Oscar hatopata uhuru kamili ambao watu wengi wanaudhania.

Oscar atatoka kwenye gereza la Atteridgeville huko Johannesburg na atasafiri maili 15 kwenda kwenye moja ya jengo la kifahari anakoishi mjomba wake huko ndani ya jiji hilo.

Mjengo huo unaomilikiwa na mjomba wake aitwaye Arnold, una ulinzi wa nyaya zenye umeme wa hali ya juu na walinzi wamemwagika ndani ya nyumba hiyo inayokadiriwa kuwa na thamani ya Pauni 10 milioni na nje yake pia.

Kwa mujibu wa chanzo kimojawapo kilichofanya mahojiano na Dail Maily ni kwamba Osca hatoruhusiwa kutoka kwenda sehemu yoyote bila ya walinzi wa nyumba hiyo.

"Watu hawajapendezwa na kuachiwa kwake, polisi Jijini Johannesburg wamepokea taarifa kwamba kuna makundi ya wahuni yamejiandaa kwa ajili ya kumlipizia juu ya kile alichokifanya kwa Reeva.

Oscar amekuwa na maadui wengi tangu afanye tukio la mauaji na kupelekwa mahakamani, baadhi walijionyesha hadharani wakati kesi yake inasikilizwa kwenye mahakama ya North Gauteng High Court mwaka 2014.

Miongoni mwa hao wawili mmoja ni mchezaji wa zamani wa mpira wa miguu  Marc Batchelor, ambaye ameshafariki dunia na mwingine ni  Mikey Schultz bado yupo hai na anajulikana kwa kazi yake ya kupewa kulipwa kwa ajili ya kuuwa.

Kuna wakati Pistorius alipokuwa nje kwa dhamana kabla ya kuhukumiwa, akiishi nyumbani kwa Arnold, alikuwa na wasiwasi juu ya maisha yake, hivyo ililazimika tahadhari kuchukuliwa.

Muda wote aliokuwepo gerezani anadaiwa alikuwa karibu na kundi la wahalifu la Chech. Pia inaelezwa alikuwa mkorofi.

Mwaka 2017 aliwahi kupata majeraha yaliyosababishwa na kupigana na mfungwa wenzake walipogombea simu.

Mbali ya hayo, inaelezwa alikuwa akisoma Biblia na kusali, pia alikuwa akiwashawishi wafungwa wenzake kumrudia Mungu.

Hali hii imezua tetesi anaweza akawa mchungaji baada ya kutoka gerezani, ikizingatiwa kwamba nyumba anayoenda kuishi ni ya waumini wa dini ya Kikristo.

Baada ya kuachiwa huru, ataendelea kufuatiliwa hadi mwaka 2029 kifungo chake kitakapomalizika.

Kwa mujibu wa mamlaka za Afrika ya Kusini, kifungo cha nje hakimfanyi Pistorius kuwa tofauti na wafungwa wengine, kwani kuna sheria itabidi azifuate ikiwa ni pamoja na kuwepo nyumbani baada ya muda fulani na kutotumia pombe na baadhi ya vinywaji.

Pia atatakiwa kufanyiwa matibabu ya kuzuia hasira na kuingizwa kwenye programu ya ukatili wa kijinsia na hatotakiwa kwenda kwenye kumbi za starehe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live