Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hata kwa totozi tuwekewe tozo?

SHOT3 Hata kwa totozi tuwekewe tozo?

Mon, 5 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mishe za ‘tauni’ zimekaa kigoroko sana hivi sasa. Hizi mbanga za tozo dizaini kama zinatufanya tuishi kwa bajeti kama Wachaga wa Mwika na Hedaru. Wakati ‘kitauni tauni’ pigo za bajeti tushazikataa kitambo hicho.

Ishu za muda na bajeti mjini hatutaki. Kutunza muda na pesa tulishindwa tangu enzi za marehemu Dito, pesa inaingia na kutoka kama ilivyo. Muda wowote tunanyanyua nanga kwenda batani bila kujali ukubwa na udogo wa bajeti.

Bongo unaondoka homu huna kitu. Unarudi usiku huna kitu pia lakini uko njwii. Yaani hatujawahi kuwa watu wa kulalamikia jambo muda mrefu. Linatoka hili kesho linaibuka lingine na wiki ijayo tunaletewa jipya. Yaani watu wa matukio.

Lakini tozo limekuwa pigo takatifu. Limefanya tuweke silaha chini. Saa moja shuka utosini na kujifanya unawaza mambo mengi ya ofisini. Watu wamekata ringi kama lori la mkaa. Tripu moja gereji moja porini.

Ukiwa na la ‘teni’ kwenye simu kwa sasa ni kama buku tu. Wanakata kwa miamala, kwa benki, kwa nauli, kwa luku. Duh! Ene wei, mambo vipi? Ishu zimekaa aje, mia mia? Au ndo filamu bado haijabadilika?

Filamu ya huenda kesho michongo itakaa on line! Kwa kesho yetu ya kila siku. Kesho ni ile ile. Kesho isiyofika. Laifu linaenda kwa matumaini kama wafuasi wa mamvi 2015. Michongo mingiii mkwanja kidogoo. Maneno mengiii, malipo kiduchu.

Advertisement Ila ‘weteva itiizi’, najua baadhi mko poa. Wengine tukisagika na vumbi la Taifa la tozo. Hii ni poa ama siyo poa? Upoa ni ule wa kupata pumzi ya Sir God bila malipo? Mjini hapa cha bure vumbi tu, mengine pesa mbele kama tai.

Najua upoa wa noti ni kitendawili tega. Gamba ni gumu! ‘Laifu’ bado kugeuka tunaungaunga sana! Okei sahau kuhusu hayo yote, ukiendelea kuwaza unaweza kupasuka bichwa na kudedi kwa mshituko wa moyo.

Ndio maana maduu ‘wanadeti’ na vizee. Hizi mbanga siyo ajabu tena. Mjukuu wa Mzee Mbonde ‘anadeti’ na Mzee Sadiq. Na Mzee Masawe babu yake Chuwa anatoka na Aneth mjukuu wa Mzee Sifael, aliyemaliza kidato cha sita juzi kati.

Siku hizi vibinti utaviona kwa ndinga ya vidingi vikienda kutafuna bata. Hata aibu havina na vizee vimekosa soni. Midomo laini kuita madingi hao bebi. Bebi? Kidingi zaidi ya mshua wako unakiita baby? Naye anaitikia ‘Yesi switii’. Aibu iliyoje!

Lakini watafanyaje. Madingi wako hoi kwa visukari wanataka liwazo la vibinti. Na vibinti viko hoi kiuchumi vinataka vitafune tozo la wastaafu. Hii kwetu uswahilini tunaita kufa kufaana. Tozo ni kama tetemeko la ardhi.

Kila mtu katikiswa, kuanzia wazee mpaka watoto. Wakati zamani bia zilinyweka kwa furaha na marafiki. Leo bia zinanyweka kwa mawazo na kitenga marafiki. Kila sehemu pesa haitoshi, kumlipia mtu nauli tu ile ya daladala unaonekana pedeshee.

Sasa usishangae pisi za mjini kwa sasa kuwekeza kwenye mioyo ya madingi. Wale madingi wako jirani na kifo kuliko uhai. Yashajenga nyumba kitambo, yalishasomesha watoto wote, hayana deni zaidi ya kula tozo la ustaafu. Pisi ndio hujiweka humo.

Mwanzo nilidhani labda ishu hizi zipo bushi tu, kumbe siyo. Hata hapa mjini mwendo ni ule ule. Huku hadi wale mademu wa kideoni, unaishia kuona swaga zao runingani. Nao mioyo yao ipo kwa madingi umri wa baba zao.

Utajiuliza ni upendo wa kweli? Ama kuna ‘samsingi else’? Kwamba ni upendo wa kweli mimi nakataa. Ndio nakataa kabisa. Najua malimbo kitaa mtasema nimeanza kuleta pigo za ‘kilong taim’. Maifuti. Mimi nahoji vitu vya msingi.

Utasikia “Umri ni namba tu”. Kama ni hivyo mbona hatuoni wakitoka na vidingi vilala hoi? Au pesa ‘zinaajasti’ umri? Hapana! Ni njaa na tamaa ndio inawapeleka kwenda kutafuna pesa za ustaafu kwa mtindo wa kitozo tozo. Havina lolote!

‘Laifu’ la ‘kupushi’ ndinga kali. Kuishi na iFone macho matatu. Kupanga ‘apatimentsi’ mitaa ya ushuani. Ndiyo msingi wa mapenzi yao kwa vizee vyenye umri wa baba zao. Kwao pesa mbele. Umri kitu gani bwana! Maisha ya tozo yanawapeleka mbio.

Vina sura nzuri lakini matendo yao. Temea mate chini. Usitemee angani maana yatakurudia mwenyewe. Toto la miaka 22 ‘kudeti’ dingi linaloitafuta 60 kama siyo laana ni nini? Tena pale sababu ya mapenzi yao inapokuwa ni tozo tu.

Kuna ‘taimu’ najiuliza, ‘kicheni pati’ zao hufundishwa jinsi ya kutafuna tozo? Au jinsi ya kutunza maisha ya ndoa? Siyo kwamba ‘nadisi’, naunga mkono kwa mlango wa nyuma. Nyie hamuoni, kutwa kwenye kumbi za pombe na vibabu vyao.

Vingine ndiyo vinaona sifa hata vinadiriki kuwatambulisha katika media, kisa? Vibabu vyenyewe ni nchi za magharibi. Vikitokewa na vilofa, utasikia vinasema. “Ujana wake ale na nani uzee wake ndiyo aje kula na mie?” Nyambafu.

Kwa vizungu vinakunjua vikisema. “Eji itizi jasti e namba.” Mwenye hela siyo babu ila lofalofa ndiyo babu. Hii yote ni kutokana na uvivu wa kufikiri.

Vibinti vingi town vivivu kufikiri. Ndio maana akili huegemeza kwa vibabu vyenye tozo la ustaafu.

Najua kuna vibinti vitanichana kuwa sina kitu ndio maana nawapondea. Lakini wapo wenye ‘bigi breini’ wa kuelewa hilo somo na kubadilika totale. Mimi niko freshi kimpango wangu, sina njaa kiviile ila nina njaa ila siyo kiviiile. Ila nina njaa.

Njaa siyo ile ya kilofalofa. Ni njaa ya mafanikio makubwa, hiyo ndio njaa yangu. Lakini senti za biere na mishe za tauni niko vyede. Kwani nikitaka pisi kali siipati? Pisi za gari na simu? Sasa mimi wa kushindwa vitu hivyo? Unanichukuliaje?

Jiangalie! Mimi naamsha akili zenu zilizolala usingizi wa pono. Kama kutaka ningetaka wake wa vibosile mnavyotoka navyo. Wale ‘wanashoo’ mapendo kinoma kwa mabaharia. Ila nakatika stimu wakituita ‘Ben Ten’. Ndio maana nawakataa.

Ila masela hatukutakiwa kulaumu sana tozo. Tozo kwetu ni kama tego ila panya. Ile michongo ya tuma na ya kutolea imekufa ‘automatikale’. ‘Hau kamzi tunablemu gavamenti’ wakati wametupa ‘asisti’ kama Aziz Kii?

Yes! Sisi masela ‘tujityuni’ na tozo lao kiroho safi. Hili halituumizi sisi, kifupi lina faida zaidi kwetu. Tozo ‘likirani ze shoo’, pisi zitalazimika kutimba mageto kufuata mapene. Badala ya zile mbanga za tuma na ya kutolea. Na hapo ndipo ‘Zawadi ya Ushindi’ tutapewa.

Tunawaambia kutuma makato yake ni makubwa kuliko tunachotuma. Kwa hiyo pisi zije geto zichukue kwa mkono keshi. Pisi zitaelewa somo. Zikitaka mapene zinajiandaa kabisa kuja mageto kwa masela.

Zinapewa kipindi cha maana ndipo zinasepeshwa kwao. Kifupi hapa ‘ze gavamenti’ imepindua meza kibabe na kutupa desa la moja kwa moja. Noma sana aiseee. Mimi pisi ikitaka mkwanja kwa sasa hakuna maelezo mengi. Aje magetoni.

Sasa akija magetoni ataamua ale kwanza ndio abebe mkwanja wangu. Au abebe mkwanja ili ale vizuri. Kazi kwake! Nina mpango wa kuandaa maandamano ya masela nchi nzima, ya kuipongeza Serikali kwa kuangalia masela kwa jicho la tatu.

Zile pigo za tuma na ya kutolea sasa zimekufa kibudu. Hakuna cha tuma na ya kutolea, wewe njoo magetoni upewe unachotaka na usichotaka kwa pamoja. Nikikutana na msela kitaa analalamikia tozo namtwanga mbata kama tatu za ghafla ghafla.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live