Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Harusi ya Wolper imeteketeza Mil. 200 na ushee

Harusi Ya Wolper Imeteketeza Mil. 200 Na Ushee Harusi ya Wolper imeteketeza Mil. 200 na ushee

Fri, 2 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mrembo Jacqueline Wolper na mumewe Rich Mitindo, hivi karibuni walifunga ndoa na kufanya sherehe ambayo imetekeza zaiidi ya shilingi milioni 200 za Kitanzania.

Akizungumza na wanahabari juzikati Wolper alisema, bado hajatulia tangu afanye tukio hilo kubwa la kihistoria kwenye maisha yake na alipoulizwa kuhusu gharama ndipo alipotaja mkwanja huo.

"Inacheza kwenye milioni 200 hivi, sisi tumefanya kitu ambacho tumeona tunakiweza, tumeridhia na watu wetu wameridhia," alisema Wolper.

Mrembo huyo alimaliza kwa kusema, wao ni wafanyabiashara hivyo hawakutumia nje ya uwezo wao wamebaki na mpunga wa kuendeleza biashara zao kama kawaida.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live