Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Harusi ya India iyohudhuriwa na Mark Zuckerberg, Rihanna na Bill Gates

Harusi Ya India Iyohudhuriwa Na Mark Zuckerberg, Rihanna Na Bill Gates Harusi ya India iyohudhuriwa na Mark Zuckerberg, Rihanna na Bill Gates

Sat, 2 Mar 2024 Chanzo: Bbc

Watu mashuhuri wenye ushawishi mkubwa duniani, akiwemo Mark Zuckerberg, Rihanna, na Bill Gates, walikusanyika katika jimbo la India la Gujarat kuhudhuria karamu ya kabla ya harusi iliyoandaliwa na mtu tajiri zaidi wa Asia.

Mukesh Ambani, mwenyekiti wa kampuni ya Reliance Industries, aliandaa tafrija ya kabla ya harusi ya mtoto wake na wageni waalikwa.

Mwanaume huyo, Anant Ambani mwenye umri wa miaka 28, amepangiwa kuoa mwanamke anayeitwa Radhika Merchant mwezi Julai.

Hafla hiyo ya siku tatu iliyofanyika Jamnagar pia itahudhuriwa na nyota wa Bollywood wakiwemo Shahrukh Khan na Amitabh Bachchan.

Kwa mujibu wa Forbes, Mukesh Ambani (umri wa miaka 66) kwa sasa ndiye mtu wa 10 tajiri zaidi duniani akiwa na utajiri wa dola bilioni 115.

Reliance Industries, iliyoanzishwa na baba yake mwaka 1966, ni shirika linalofanya kazi katika nyanja mbalimbali ikiwa ni pamoja na kusafisha mafuta, uuzaji wa bidhaa mbali mbali za rejareja, kutoa huduma za kifedha, na mawasiliano ya simu.

Watoto wake wote watatu ni wajumbe wa bodi ya wakurugenzi wa kampuni hiyo, huku Anant Ambani akiwa ndiye mdogo zaidi.

Kijana huyo mwenye umri wa miaka 28 anajihusisha na biashara ya nishati ya Reliance na pia anahudumu kama mjumbe wa bodi ya wakfu wa kampuni hiyo.

Hafla hii ya kabla ya sherehe ilifanywa kwa mujibu wa utamaduni wa familia ya Ambani kuandaa karamu ya kifahari ya harusi.

Chanzo: Bbc