Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Harmorapa amgomea Harmonize "Haiwezi kutokea"

40407 Harmopic Harmorapa amgomea Harmonize "Haiwezi kutokea"

Thu, 11 Jun 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kufuatia madai ya kublokiwa kwenye mtandao wa Instagram na msanii Harmonize, Harmorapa amekataa kumuomba msamaha ili kwenda sawa, kwa kusema suala hilo haliwezi kutokea kwani hakuna jambo ambalo amemkosea.

Akizungumza kwenye mahojiano ya EATV & EA Radio Digital, Harmorapa amesema kuwa suala la kublokiwa na Harmonize lina stori ndefu na hawezi kulizungumzia kwa sasa ila ikifika muda ataweka wazi kila kitu.

"Siwezi kukaa kumuomba msamaha kwa sababu, sidhani kama kuna jambo nimemkosea, kwanza kila mtu ananyota yake na siwezi kutembelea nyota ya mtu, Mungu aliyeniumba mimi ndiyo kamuumba yeye na watu wote, kwahiyo haiwezi kutokea kumuomba msamaha kisa nimetembelea nyota yake na sijamkosea kama ningemkosea ningemuomba msamaha, hata mimi nilikuwa na upepo wangu" ameeleza Harmorapa

Chanzo: www.tanzaniaweb.live