Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Harmonize yupo mbele ya muda

Harmonize Hits Harmonize yupo mbele ya muda

Tue, 7 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Umetimia mwaka mmoja tangu Harmonize alipoiachia albamu yake ya ‘MadeFor Us’, ambayo ilikuja na nyimbo 14 zikiwemo ‘Wote’, ‘Nitaubeba’, ‘Best Friend’ na ‘Amelowa’.

Made For Us iliachiwa Oktoba 28, 2022 ikiwa ni albamu ya tatu kutoka kwa Boss huyo wa Konde Gang. Albamu hiyo ni mchanganyiko wa nyimbo zilizotengenezwa na waandaaji tofauti ambao ni Dj Tarico, Daxo Chali, Paul Maker, B Boy Beats, Sign Beat na Gachi B.

Albamu hiyo ina nyimbo 14, lakini ni nyimbo sita pekee ambazo Harmonize aliwashirikisha marafiki na washirika wenzake; ambao ni Abigail Chams, Mabantu, Alice Kella, Spice, Bruce Melodie na Nak.

Kabla ya albamu hiyo kutolewa, Harmonize alikuwa ametoka kuachia nyimbo mbili, ‘Bakhresa’ na ‘Mdomo’ ambayo alimshirikisha Ibraah, nyimbo hizo mbili zilitolewa baada ya mafanikio ya albamu ya pili ya Harmonize ‘High School’ ya mwaka 2021, iliyokuwa inaifuatia albamu yake ya kwanza ‘Afro East’ -ambayo iliachiwa mwaka 2020, baada ya Harmonize kuitangazia jamii ya Bongo Fleva kuwa, mkataba wake na WCB ulitenguliwa.

Kabla ya ‘Made For Us’ kutolewa, Harmonize aliziachia ‘Leave Me Alone’ ft. Abigail Chams, ‘You’, ‘Deka’ ft Mabantu, ‘Miss Bantu’ ft. Spice, ‘Amelowa’ na ‘Nitaubeba’ kama lead singles.

Leave Me Alone aliyoshirikiana na Abigail Chams ni miongoni kati ya nyimbo za Harmonize zilizopokelewa kwa matokeo chanya kwenye jamii ya wapenda muziki kwa nyakati kadhaa mwishoni mwa mwaka 2022 kuja mwanzoni mwa mwaka 2023.

Video ya wimbo ‘Nitaubeba’, ilipambwa na sura ya Kajala, aliyekuwa mpenzi wa Harmonize wakati huo, anayedhaniwa kuwa albamu hiyo ilifanywa maalum kwa ajili ya mapenzi yao.

Ilipotolewa video ya ‘Amelowa’, Harmonize alihusishwa kwenye drama iliyomuhusu ‘Sophy’, video vixen aliyejitoa fahamu na kufanya michezo ya kishubwada kwenye video ya wimbo huo, ambao pia Harmonize aliutengenezea remix wimbo na kuunda wimbo wa ushabiki wa Yanga ulioitwa ‘Wamelowa’.

Video ya wimbo mwingine iliyoleta mastori mengi kutoka kwenye ‘Made For Us’, ni video ya ‘Wote.’ Hii ni moja kati ya video za kibabe zilizowahi kufanywa na wasanii wa Bongofleva.

Video ya ‘Wote’ ilienda viral muda mfupi kabla ya kutolewa, hiyo ilitokea baada ya video na picha za Harmonize kuonekana kwenye mikao ya kimahaba na mrembo Feza Kessy.

Baada ya video hiyo kutolewa, tukapata majibu ya maswali yetu kuhusu wawili hao kutokuwa wapenzi bali ilikuwa ni seemu ya utengenezaji wa video ya ‘Wote’.

Wote ni wimbo mwingine wa Harmonize uliopokelewa kwa matokeo chanya sana. Licha ya albamu ya Made For Us kuachiwa Oktoba mwaka 2022, ‘Wote’ ilikuja kupata umaarufu katikati ya mwaka 2023 baada ya kuachiwa video yake Januari mwaka huu.

Made For Us ilichaguliwa kuwania tuzo za muziki Tanzania, kwenye kipengele cha albamu bora ya mwaka ambapo albamu ya Barnaba – Love Sounds Different, ilichaguliwa kushinda.

Video ya ‘Just The Way You Are’ ambayo ni kolabo na Bruce Melodie na Nak, haikufanya vizuri sana, kwa kipindi cha miezi kumi na moja video hiyo imetazamwa mara laki sita tu. Video ya Miss Bantu na Spice ndiyo ya mwisho kuachiwa kutoka kwenye albamu hiyo.

Made For Us imeweka rekodi ya kuwa albamu bora Tanzania kwa muda mrefu, Kwenye Boom Play Tanzania, albamu hiyo imekuwa namba moja kwa wiki nyingi tofauti mwaka huu, huku Harmonize akiwa msanii mwenye albamu mbili kwenye kumi bora ya albamu za kila wiki BoomPlay.

Albamu hiyo inampa ubabe Harmonize kwa kutufanya tumtaje kwa ujasiri kama msanii wa Bongo fleva wa kizazi hiki ambaye amekuwa na uthubutu wa kuachia albamu tatu mfululizo.

Kitendo cha Harmonize kufanya albamu tatu kwa miaka mitatu mfululizo, kilitafsriwa na wakosoaji kama kukurupuka, kukosa ushauri mzuri na kushindwa kuwa na mkakati mzuri wa kuachia kazi zake. Made For Us imethibitisa ushujaa wa Harmonize kwa kubadili kile kilichoitwa kukurupuka hadi kumiliki chati kwa mwaka mzima.

Kupitia ‘Made For Us’, Harmonize na mashabiki wameithibitishia Industry kwa kutuaminisha movement ya albamu za back to back kutoka kwa msanii mmoja inawezekana kufanyika na mashabiki wakaunga mkono arakati hiyo.

Katika kipindi cha mwaka mmoja, ‘Made For Us’ imesikilizwa takribani mara milioni 180 kwenye majukwaa yote ya kusikilizisha muziki, matoleo yote ya YouTube kwa maana ya audio, lyrics na official music video, yanakusanya zaidi ya watazamaji milioni 165.

Baada ya Made For Us, Harmonize ameendelea kuachia nyimbo nyingine mwaka huu zikiwemo ‘Dear Ex’, ‘Hawaniwezi’ na ‘Single Again’, wimbo ambao unatajwa kuwa wimbo wa Bongo fleva uliosikilizwa mara nyingi zaid mwaka huu.

Kwa sasa, Harmonize anatamba na ‘Sijalewa’, wimbo mpya ambao ameuachia wiki mbili baada ya kutangaza ujio wa albamu zake mbili za mwisho kabla aache kufanya albamu na kuligeukia soko la singo, kwa kile alichokiita kukosekana kwa upinzani kwenye soko la albamu.

Harmonize ametangaza ‘Visit Bongo’ kama jina la albamu yake inayofuata baada ya ‘Made For Us’.

Tangazo la Harmonize kuitambulisha albamu mpya mwaka mmoja baada ya Made For Us, ni uthibitisho kwamba, moto wa Harmonize haupoi, visit Bongo itakuwa albamu ya nne mfululizo kutokea kwa Harmonize ; kumaanisha Harmonize yuko mbele ya muda kwenye kuutafuta na kuumiliki ufalme wa soko la albamu za muziki Tanzania.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live