Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Harmonize mguu ndani mguu nje Wasafi

71866 Harmonize+pic

Sat, 17 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Kuna ukweli wowote kuhusu habari zinazosambaa katika mitandao ya kijamii kuwa msanii Harmonize amejiengua katika lebo ya Wasafi inayoongozwa na Diamond Platnumz.

Hakuna anayejua hilo lakini kuna baadhi ya kauli  zilizotolewa na Diamond mwenyewe na mmoja wa mameneja wake zinaweza kutoa picha ingawa hakuna kati yao aliyethibitisha kuwa Harmonize ameachana na lebo hiyo.

 “Kama Harmonize anataka kuondoka aondoke,” alinukuliwa akisema Diamond na baadaye kauli hiyo kuungwa mkono na mmoja wa  mameneja wa Wasafi, Said Fella, “Kama akiamua kuondoka hakuna wa kumzuia.”

Huo ni mwanzo wa kile kinachodaiwa Harmonize anaweza kujitoa kwenye lebo ya Wasafi.

Lakini mara kadhaa Harmonize amekuwa akijibu kuhusu tetesi hizo, “Siwezi kuondoka Wasafi kwani namchukulia  Diamond kama baba yangu ndio aliyenilea kimuziki.”

Tayari Harmonize anamiliki lebo ya muziki ya Konde Gang ambayo inafanya kazi zake kama ilivyo Wasafi.

Pia Soma

Kuna baadhi ya maeneo ambayo amekuwa akienda kufanya shughuli za kijamii bila kuambatana na wasanii wenzake wa Wasafi.

Hivi karibuni Harmonize katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram aliondoa utambulisho  wake kuwa chini ya Wasafi.

Kabla ya kuondoa utambulisho huo ilikuwa ikisomeka ‘Signed Under WCB Wasafi’  sasa ameondoa neno hilo na kuandika ‘WCB4LIFE’.

Harmonize hakuwepo katika ufunguzi wa tamasha la Wasafi lililofanyika Julai 19, 2019 katika Viwanja vya Zimbihile, Muleba mkoani Kagera  na badala yake alijiunga nao jijini Mwanza kwa madai kuwa alikuwa na shoo nje ya nchi.

Chanzo: mwananchi.co.tz